Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

DR MANGURUWE ATANGAZA NAFASI ZA KAZI KWA VIJANA WENYE VIPAJI


Mkurugenzi wa mradi mkubwa wa Dr. Manguruwe Project ametangaza nafasi za kazi katika fani mbalimbali akiwa shambani kwenye mradi  huo  uliopo Zamahero Dodoma lengo kuu likiwa ni kuibua vipaji na kusaidia vijana kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine.


 Dr. Manguruwe amesema kuwa vipaji hivyo ikiwa ni pamoja na kuigiza, kuimba, kuchekesha, ngumi, sarakasi, kucheza n.k itafanyika kwa kuwashindanisha vijana na watakaoshinda basi watapata nafasi ama fursa ya kuwa katika mradi wake wakifanya kazi kama ajira na pia kutumia muda maalumu kutengeneza maudhui ya mitandaoni ili kuendeleza vipaji.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com