Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

WANAWAKE WASHAURIWA KUFUGA NYUKI, KUPANDA MITI BIASHARA KUJIINUA KIUCHUMI, KUKABILIANA MABADILIKO YA TABIANCHI

Mhifadhi wa  Wakala wa Misitu Tanzania (TFS), Zuberi Mabie akihamasisha wanawake kufuga nyuki ili kuzalisha asali wakati wa warsha ya Teknolojia na mabadiliko ya tabia nchi iliyofanyika leo Jumatano Agosti 28,2024 wakati wa Tamasha la 7 la Jinsia Ngazi ya Wilaya 2024  

Na Mwandishi Wetu - Malunde Media

Wanawake wametakiwa kuchangamkia fursa zinazopatikana katika misitu ikiwemo ufugaji nyuki ili kujikwamua kiuchumi na kutunza mazingira ili kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

Ushauri huo umetolewa na Mhifadhi wa  Wakala wa Misitu Tanzania (TFS), Zuberi Mabie wakati wa warsha ya Teknolojia na mabadiliko ya tabia nchi iliyofanyika leo Jumatano Agosti 28,2024 wakati wa Tamasha la 7 la Jinsia Ngazi ya Wilaya 2024  linalofanyika katika Viwanja vya Sabasaba Kondoa Mkoani Dodoma.

Mabie ameshauri wanawake wafanye shughuli Rafiki kwa mazingira ikiwemo ufugaji wa nyuki na kupanda miti ya kibiashara kupitia vikundi vyao huku akihamasisha wanawake kuingia kwenye kamati za mazingira za vijiji ili kubeba zaidi ajenda ya utunzaji mazingira.

“Wanawake waziendee shughuli za misitu na miradi Rafiki kwa mazingira ili kujiinua kiuchumi na kutunza mazingira kwa kufuga nyuki ili kuzalisha asali kwa sababu mahitaji ya asali nchini ni makubwa lakini pia soko la asali nje ya nchi ni kubwa”,amesema Mabie.

“Mabadiliko ya tabia nchi yanamuathiri mwanamke kutokana na kwamba changamoto za mabadiliko ya tabia nchi yanasababisha ukame, ukosefu wa chakula na mmomonyoko wa ardhi. Ukame unamfanya mwanamke akose chakula hivyo atashindwa kuhudumia familia na atatumia muda mwingi kutafuta chakula na kutafuta huduma ya maji huku mmomonyoko wa ardhi utasababisha ashindwe  kupata chakula”,ameongeza Mabie.

Aidha ameshauri wananchi kuendelea kutumia nishati safi ikiwemo matumizi ya gesi ili kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

 Kwa upande wake, Joyce Elias kutoka Kituo cha Taarifa na Maarifa Mamire Babati Mkoani Manyara amewashauri wananchi kuchangamkia Kilimo Ikolojia kinachohusisha mwingiliano wa binadamu, mimea na mifugo kwani ni kilimo cha asili salama kwa gharama ndogo.

Mhifadhi wa  Wakala wa Misitu Tanzania (TFS), Zuberi Mabie akielezea kuhusu Teknolojia na mabadiliko ya tabia nchi wakati wa warsha ya Teknolojia na mabadiliko ya tabia nchi wakati wa Tamasha la 7 la Jinsia Ngazi ya Wilaya 2024 

Joyce Elias kutoka Kituo cha Taarifa na Maarifa Mamire Babati Mkoani Manyara akielezea kuhusu Kilimo Ikolojia
Joyce Elias kutoka Kituo cha Taarifa na Maarifa Mamire Babati Mkoani Manyara akielezea kuhusu Kilimo Ikolojia
Mratibu wa Mradi wa LDFS Kondoa (GEF) IPAD , Isaack Luambano akizungumza wakati wa warsha ya Teknolojia na mabadiliko ya tabia nchi wakati wa Tamasha la 7 la Jinsia Ngazi ya Wilaya 2024 

Mhifadhi Msaidizi TFS, Makaya Malila akielezea kuhusu ufugaji nyuki wakati wa warsha ya Teknolojia na mabadiliko ya tabia nchi wakati wa Tamasha la 7 la Jinsia Ngazi ya Wilaya 2024 

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com