Na Marco Maduhu,SHINYANGA
MWENGE wa uhuru umewasili mkoani Shinyanga ambapo utakimbizwa kilomita 643.2 na kupita kwenye miradi 46 ya maendeleo yenye thamani ya Sh.bilioni 26.4
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Anamringi Macha akizungumza wakati wa kutoa salamu za mwenge wa uhuru, mara baada ya kukabidhiwa na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Kenani Kihongosi, amesema mkoa huo umejipanga vyema kuukimbiza mwenge huo na miradi yote iko vizuri.
Aidha,amesema katika suala la utunzaji wa mazingira mkoa huo katika mwaka wa fedha 2023/2024 wamepanda miti milioni 5.8
Pia,ametoa wito kwa wananchi wajitokeze kwa wingi kushiriki kwenye uchaguzi wa Serikali za mitaa, pamoja na kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la mpiga kura.
Mwenge huo wa uhuru mkoani Shinyanga utaanza kukimbizwa wilayani Kishapu Kilomita 91.3 na utapita kwenye miradi 10 ya maendeleo, kuzindua, kuona na kuweka jiwe la msingi yenye thamani ya sh.bilioni 3.5
Kauli mbiu ya mbio za mwenge wa uhuru kitaifa 2024 inasema"Tunza Mazingira na Shiriki uchaguzi wa Serikali za mitaa kwa ujenzi wa taifa endelevu".
Social Plugin