AWESO ATEMBELEA BANDA LA SEKTA YA MAJI NANE NANE, APONGEZA ATOA MAAGIZO YA UBORESHAJI HUDUMA



Na Christina Cosmas, Morogoro

Waziri wa Maji Jumaa Aweso amepongeza ushirikiano baina ya Taasisi za sekta ya Maji Morogoro na kuzitaka kuendelea kushirikiana katika kuhakikisha lengo la kutoa huduma ya maji ya uhakika kwa wananchi wa Morogoro linatimia.


Waziri Aweso amesema hayo leo alipotembelea banda la sekta ya maji Morogoro katika maonesho ya Nane nane Kanda ya Mashariki yanayoendelea katika viwanja vya Nane Nane Taso, Morogoro.


Aweso ameiasa MORUWASA kuhakikisha kuanzia kesho wanalala saiti ili kuhakikisha malalamiko ya maji kwa maeneo ya Lukobe, Mkundi, Mindu na Mkambarani yanapata huduma ya majisafi na salama.

"Maelekezo ambayo nimeyatoa kwa menejimenti ya MORUWASA lakini pia na Bodi ya MORUWASA kupitia Mkurugenzi wa MORUWASA Injinia Tamim kuanzia kesho na kuendelea ,watalala wataamka maeneo hayo ambayo nimeyataja kuhakikisha wanaongeza nguvu maeneo hayo waweze kupata huduma ya maji safi na salama", amesema Aweso.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post