Wakulima kutoka maeneo mbalimbali ya jiji la Mwanza wameonesha kuridhishwa na ustawi na uzaaji wa mbegu mbalimbali zilizopandwa kwenye mashamba madogo ya mfano katika viwanja vya maonesho ya nanenane, Nyamhongolo.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti na watafiti wa kituo cha Ukiriguru, wamesema baadhi ya mbegu kama migomba, mbaazi, na viazi vitamu waliyozoea kupanda imeonekana kuwa na uzaaji hafifu na kwamba ustawi na uzaaji wa mbegu za TARI umewapa hamasa ya kutumia mbegu bora.
Kutokana na hamasa hiyo, watafiti wametumia fursa hiyo kutoa utaratibu mzuri wa namna ya kuzipata mbegu bora kutoka vituo mbambali vya TARI vilivyopo maeneo mengi nchini.
Katika maonesho ya nanenane yanayoendelea katika viwanja vya Nyamhongolo, wananchi wa rika mbalimbali wanapata fursa ya kujifunza na kuona teknolojia za mazao tofauti kutoka kwa watafiti.
Miongoni mwa teknolojia ambazo zimewavutia wananchi wengi ni teknolojia ya sukuma vuta (Push-pull technology) pamoja na upandaji wa mazao kwa nafasi.
Social Plugin