TK MOVEMENT YAHAMASISHA WANA-CHALINZE KUCHANGAMKIA FURSA


Kutoka kushoto ni Mratibu Msaidizi wa TK Movement halmashauri ya Chalinze,katikati ni Katibu mtendaji wa TK Movement Bw. Nelson Fredrick na kushoto ni Mratibu wa TK Movement Bi. Jamila Juma


NA. ELISANTE KINDULU,  CHALINZE

JUMUIYA ya Taifa letu, Kesho yetu, maarufu TK Movement imewahamasisha wana Chalinze kuvumbua miradi ya kiuchumi na kuchangamkia fursa mbalimbali ndani na nje ya halmashauri yao. 

Hayo yamesemwa na Katibu mtendaji wa TK Movement mkoa wa Pwani Bw. Nelson Fredrick alipowatembelea wana jumuiya hiyo na kuzungumza nao katika viwanja vya shule ya msingi Chalinze leo tarehe 31.8.2024.

Bw. Fredrick amesema jumuiya hiyo ina kazi kubwa ya kuhamasisha jamii kujikomboa kiuchumi katika kuhamasisha vikundi vya uzalishaji mali ikiwemo kuomba mikopo itakayotolewa na halmashauri pamoja na kusaidia upatikanaji wa fursa mbalimbali kwa vijana, wanawake na makundi maalumu bila kujali tofauti zao za kidini, itikadi ya kisiasa, ukabila ama ukanda.

Mapema akizungumza na wanajumuiya hiyo, Diwani wa kata ya Pera katika halmashauri ya Chalinze, Mh. Jackson Mkango ameipongeza TK Movement kwa malengo Yao mazuri na ameahidi kutoa ushirikiano pale itakapohitajika.

Kikao hicho pia kilihudhuriwa na Mratibu wa jumuiya hiyo wa halmashauri ya Chalinze  Bi. Jamila Juma, Mratibu Msaidizi Bi. Christina Emmanuel pamoja na wadau mbalimbali wa maendeleo.



Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post