Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

INEC YAENDESHA MAFUNZO KWA WASIMAMIZI WA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA MKOA WA SHINYANGA

Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog

Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) imetoa mafunzo ya Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kwa Mratibu wa Uandikishaji Mkoa wa Shinyanga, Maafisa waandikishaji, Maafisa Waandikishaji Wasaidizi ngazi ya Jimbo, Maafisa Uchaguzi, Maafisa Ugavi na Maafisa TEHAMA wa Halmashauri za Mkoa wa Shinyanga.

Akizungumza wakati akifungua mafunzo hayo leo Jumamosi Agosti 10,2024, Makamu Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufaa (Mstaafu), Mbarouk Salim Mbarouk amesema washiriki wa mafunzo hayo wameteuliwa na Tume kuendesha na kusimamia zoezi la uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura.

Amesema mafunzo hayo yanahusisha namna ya ujazaji wa fomu pamoja na kutumia mfumo wa kuandikisha wapiga kura (Voters Registration System – VRS) ili waweze kupata uelewa wa pamoja utakaowapa fursa ya kutumia kwa ufasaha mfumo huo pamoja na vifaa vingine vya kuandikisha wapiga kura.
Mratibu wa Uandikishaji Mkoa wa Shinyanga, Maafisa waandikishaji, Maafisa Waandikishaji Wasaidizi ngazi ya Jimbo, Maafisa Uchaguzi, Maafisa Ugavi na Maafisa TEHAMA wa Halmashauri za Mkoa wa Shinyanga wakila kiapo cha kutunza siri na tamko la kujitoa uanachama au kutokuwa mwanachama wa chama chochote cha siasa wakati wa kutekeleza majukumu yao.

“Kuteuliwa kwenu kunatokana na ujuzi, uwezo na weledi mlionao katika kutekeleza majukumu ya kitaifa likiwemo zoezi la uboreshaji wa daftari ikiwa ni maandalizi ya uchaguzi mkuu 2025. Ni matarajio ya tume kuwa kutokana na mafunzo haya mtapata elimu na ujuzi wa kutosha utakaowawezesha kutekeleza majukumu yenu ili kufanikisha zoezi la uboreshaji”,amesema Mhe. Jaji wa Rufaa (Mstaafu).

“Mafunzo haya yanawajengea umahiri wa kuwafundisha maafisa waandikishaji wasaidizi ngazi ya kata kisha nao watatoa mafunzo hayo kwa waendeshaji wa vifaa vya Bayometriki na Waandishi Wasaidizi ambao ndio watahusika na uandikishaji wa kura vituoni”,ameeleza.

Mhe. Jaji wa Rufaa (Mstaafu) ameongeza kuwa, maafisa TEHAMA watapatiwa mafunzo maalumu jinsi ya kukabiliana na changamoto mbalimbali za kiufundi (Troubleshooting) endapo zitajitokeza wakati wa zoezi la uandikishaji wa wapiga kura.
Makamu Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufaa (Mstaafu), Mbarouk Salim Mbarouk.

Aidha amesema matokeo bora ya zoezi hilo yanategemea uwepo wa ushirikiano mkubwa kati ya watendaji wote wa uboreshaji, serikali, vyama vya siasa na wadau wengine wa uchaguzi.

Katika hatua nyingine amebainisha kuwa, wakati wa uboreshaji wa daftari la wapiga kura, Mawakala wa vyama vya siasa wataruhusiwa kuwepo katika vituo vya kuandikisha wapiga kura hali itakayosaidia kuleta uwazi katika zoezi zima ambapo mawakala hao watasaidia kutambua waombaji wa eneo husika hivyo kupunguza kutokea kwa vurugu zisizokuwa za lazima.

“Pia tume imetoa kibali cha kutoa elimu ya mpiga kura wakati wa uboreshaji wa daftari kwa asasi za kiraia 157 na asasi za kiraia 33 kwa ajili ya uangalizi wa zoezi hili la uboreshaji wa daftari la wapiga kura likiongozwa na kauli mbiu isemayo ‘Kujiandikisha kuwa mpiga kura ni msingi wa uchaguzi bora”,ameongeza.
Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura Mkoani Shinyanga utafanyika sambamba na Mkoa wa Mwanza kuanzia tarehe 21 hadi 27, Agosti, 2024 ambapo vituo vitafunguliwa saa 02:00 asubuhi na kufungwa saa 12:00 jioni.

Kwa Mkoa wa Shinyanga, Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi inatarajia kuandikisha wapiga kura wapya 209,951 ikiwa ni ongezeko la asilimia 21 ya wapiga kura 995,918 waliopo kwenye daftari la kudumu la wapiga kura ambapo Tume inatarajia baada ya uandikishaji, Mkoa wa Shinyanga utakuwa na wapiga kura 1,205,869.

Vituo 40,126 vya kuandikisha wapiga kura vitatumika katika uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura mwaka 2024 ambapo kwa Mkoa wa Shinyanga kuna vituo 1,339 vitakavyotumika kwenye uboreshaji kwa mwaka huu ikiwa ni ongezeko la vituo 122 katika vituo 1,217 vilivyotumika kwenye uboreshaji mwaka 2019/20.

ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Makamu Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufaa (Mstaafu), Mbarouk Salim Mbarouk akizungumza wakati akifungua mafunzo ya Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kwa Mratibu wa Uandikishaji Mkoa wa Shinyanga, Maafisa waandikishaji, Maafisa Waandikishaji Wasaidizi ngazi ya Jimbo, Maafisa Uchaguzi, Maafisa Ugavi na Maafisa TEHAMA wa Halmashauri za Mkoa wa Shinyanga leo Jumamosi Agosti 10,2024 -Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Makamu Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufaa (Mstaafu), Mbarouk Salim Mbarouk akizungumza wakati akifungua mafunzo ya Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kwa Mratibu wa Uandikishaji Mkoa wa Shinyanga, Maafisa waandikishaji, Maafisa Waandikishaji Wasaidizi ngazi ya Jimbo, Maafisa Uchaguzi, Maafisa Ugavi na Maafisa TEHAMA wa Halmashauri za Mkoa wa Shinyanga

Mkurugenzi wa Habari na Elimu ya Mpiga Kura wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi Bi. Giveness Aswile akizungumza wakati wa mafunzo hayo kwa niaba ya Mkurugenzi wa Uchaguzi
Mkurugenzi wa Habari na Elimu ya Mpiga Kura wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi Bi. Giveness Aswile akizungumza wakati wa mafunzo hayo kwa niaba ya Mkurugenzi wa Uchaguzi
Hakimu Mkazi, Mhe. Goodselda Charles Kalumuna akielezea kuhusu kiapo cha kutunza siri na tamko la kujitoa uanachama au kutokuwa mwanachama wa chama chochote cha siasa kwa Mratibu wa Uandikishaji Mkoa wa Shinyanga, Maafisa waandikishaji, Maafisa Waandikishaji Wasaidizi ngazi ya Jimbo, Maafisa Uchaguzi, Maafisa Ugavi na Maafisa TEHAMA wa Halmashauri za Mkoa wa Shinyanga wakati wa kutekeleza majukumu yao
Mratibu wa Uandikishaji Mkoa wa Shinyanga, Maafisa waandikishaji, Maafisa Waandikishaji Wasaidizi ngazi ya Jimbo, Maafisa Uchaguzi, Maafisa Ugavi na Maafisa TEHAMA wa Halmashauri za Mkoa wa Shinyanga wakila kiapo cha kutunza siri na tamko la kujitoa uanachama au kutokuwa mwanachama wa chama chochote cha siasa wakati wa kutekeleza majukumu yao

Naibu Afisa Uhamiaji Mkoa wa Shinyanga SI. Lydia Angumbwike Mwamsiku akitoa elimu ya Uraia kwa Mratibu wa Uandikishaji Mkoa wa Shinyanga, Maafisa waandikishaji, Maafisa Waandikishaji Wasaidizi ngazi ya Jimbo, Maafisa Uchaguzi, Maafisa Ugavi na Maafisa TEHAMA wa Halmashauri za Mkoa wa Shinyanga
Maafisa waandikishaji, Maafisa Waandikishaji Wasaidizi ngazi ya Jimbo, Maafisa Uchaguzi, Maafisa Ugavi na Maafisa TEHAMA wa Halmashauri za Mkoa wa Shinyanga wakiwa kwenye mafunzo

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com