Polisi na wananchi
Shughuli za wananchi wa Kata ya Lamadi wilayani Busega, mkoani Simiyu, zimesimama tangu asubuhi, baada ya wananchi kuandamana katika kituo cha polisi cha Lamadi kwa madai ya kukithiri kwa matukio ya watoto kupotea katika mazingira yasiyojulikana.
Hali hiyo imepelekea wananchi kufunga barabara kuu, inayounganisha mikoa mitatu ya Mwanza, Simiyu na Mara, huku wakiyashambulia magari yanayopita barabani kwa mawe wakidai wamechoshwa na matukio hayo.
Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Simiyu, inayoongozwa na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Simon Simalenga, imefika katika eneo hilo na kuimarisha usalama kwa kuwatawanya wananchi hao kwa kupiga mabomu ya machozi.
Chanzo- EATV