Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na chuo cha Stony Brook University kutokea nchini Marekani, ulionesha asilimia 32 ya watu ambao walikumbwa na upweke wa kupitiliza walikuwa kwenye asilimia kubwa ya kukatisha maisha yao.
Avi Schiffmann, amekuja na majibu ya watu ambao hukumbana na upweke kwa kuja na kifaa kinachoitwa ‘’FRIEND’’ kifaa hichi kilichotengenezwa kwa akili mnemba kinakuwezesha kuungana na wewe kihisia kwa kusikiliza mazungumzo yako na kukushauri na kukupa moyo pale panapowezekana kwa njia ya maandishi.
Kinavyofanya kazi kifaa hiki, unakivaa shingoni alafu moja kwa moja unakinganisha na simu janja yako, baada ya hapo kinakuwezesha kukupa majibu ya changamoto unazungumbana nazo kwenye mizunguko ya kila siku na kwenye hali ambayo unajihisi upweke.
Ukihitaji kifaa hichi cha ‘’FRIEND’’ basi utahitajika kukinunua kwa kiasi cha shilingi laki mbili kwa pesa ya Tanzania.