INEC YAKUTANA NA WADAU WA UCHAGUZI SHINYANGA... UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA KUFANYIKA AGOSTI 21-27,2024

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) imekutana na Wadau wa Uchaguzi Mkoa wa Shinyanga kwa ajili Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Mpiga Kura linalotarajiwa kufanyika tarehe 21- 27/8/2024 mkoani humo likiongozwa na kauli mbiu 'Kujiandikisha kuwa mpiga kura ni msingi wa uchaguzi bora'.

Miongoni mwa wadau walioshiriki kwenye mkutano huo ni Viongozi wa vyama vya siasa, Viongozi wa Dini, Wawakilishi wa Asasi za Kiraia, Wahariri wa Vyombo vya habari, Waandishi wa habari, Maafisa Habari wa Mkoa na Halmashauri, Wawakilishi wa Makundi mbalimbali ya Vijana, Watu wenye ulemavu, Wanawake na Wazee wa Kimila.

Akizungumza wakati akifungua mkutano huo uliofanyika leo Ijumaa Agosti 9,2024 Makamu Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufaa (Mstaafu), Mbarouk Salim Mbarouk amesema mkutano huo umelenga kupeana taarifa mbalimbali za maandalizi kwa ajili ya kuanza rasmi kwa zoezi la uboreshaji wa Daftari la kudumu la wapiga kura.

“Lengo la kukutana na wadau hawa ni kupeana taarifa za uwepo wa zoezi hili na kuwapitisha katika vifaa na mifumo ya uandikishaji pamoja na kuona namna zoezi litakavyofanyika vituoni. Tume imekutana na wadau ili kupeana taarifa juu ya maandalizi ya Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura na maandalizi hayo pamoja na mambo mengine yanajumuisha uhakiki wa vituo vya kuandikisha wapiga kura, uboreshaji wa majaribio, ununuzi wa vifaa na ushirikishwaji wa wadau”, amesema Mhe. Jaji wa Rufaa (Mstaafu) Mbarouk.

Aidha ametoa wito kwa wananchi wajitokeze kwa wingi kwenye vituo ili kuboresha taarifa zao kwenye daftari la kudumu la mpiga kura, huku ikitoa tahadhari kwao wasijiandikishe mara mbili watakaobainika watachukuliwa hatua kali za kisheria kwa kulipa faini au kufungwa jela.

“Kujiandikisha zaidi ya mara moja kwenye uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura ni kosa kisheria na adhabu yake ni faini ya Shilingi 100,000/= hadi 300,000/=  na kifungo ni miezi 6 hadi miaka 2 au vyote kwa pamoja”, amesema Jaji Mstaafu Mbarouk.

Mkurugenzi wa Kitengo cha Huduma za Kisheria wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Bw. Seleman Mtibora ambaye amewasilisha mada kwa niaba ya Mkurugenzi wa Uchaguzi mkoani Shinyanga,
amefafanua kuwa, kwa kuzingatia Matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022, wapiga kura 5,586,433 wapya wanatarajiwa kuandikishwa sawa na asilimia 18.7 ya wapiga kura 29,754,699 waliopo kwenye daftari baada ya uboreshaji uliofanyika mwaka 2019/20 na kwamba wapiga kura 4,369,531 inatarajiwa wataboresha taarifa zao.

"Kwa Mkoa wa Shinyanga, Tume inatarajia kuandikisha wapiga kura wapya 209,951 ikiwa ni ongezeko la asilimia 21 ya wapiga kura 995,918 waliopo kwenye daftari la kudumu la wapiga kura ambapo Tume inatarajia baada ya uandikishaji Mkoa wa Shinyanga utakuwa na wapiga kura 1,205,869. 

"Vituo 40,126 vya kuandikisha wapiga kura vitatumika katika uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura mwaka 2024 ambapo kwa Mkoa wa Shinyanga kuna vituo 1,339 vitakavyotumika kwenye uboreshaji kwa mwaka huu ikiwa ni ongezeko la vituo 122 katika vituo 1,217 vilivyotumika kwenye uboreshaji mwaka 2019/20",ameongeza Mtibora.

Uzinduzi wa zoezi la uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura ulifanyika mkoani Kigoma tarehe 20 Julai, 2024 na mgeni rasmi alikuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (MB) ambapo ulienda sambamba na kuanza kwa mzunguko wa kwanza wa uboreshaji kwenye mikoa mitatu ya Kigoma, Tabora na Katavi na kufuatiwa na mzunguko wa pili umejumuisha mikoa ya Geita na Kagera. 

Kwa sasa, uboreshaji wa Daftari unaendelea kwenye mikoa hiyo ya Kagera na Geita hadi tarehe 11 Agosti, 2024 ambapo vituo vinafunguliwa kuanzia saa 2:00 asubuhi na kufungwa saa 12:00 jioni.
Makamu Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufaa (Mstaafu), Mbarouk Salim Mbarouk akizungumza wakati akifungua Mkutano wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi na Wadau wa Uchaguzi Mkoa wa Shinyanga kwa ajili Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Mpiga Kura leo Ijumaa Agosti 9,2024 katika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga - Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Makamu Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufaa (Mstaafu), Mbarouk Salim Mbarouk akizungumza wakati akifungua Mkutano wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi na Wadau wa Uchaguzi Mkoa wa Shinyanga kwa ajili Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Mpiga Kura

Mkurugenzi wa Habari na Elimu ya Mpiga Kura wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi Bi. Giveness Aswile akizungumza wakati wa mkutano wa Tume na Wadau wa Uchaguzi Mkoa wa Shinyanga
Mkurugenzi wa Habari na Elimu ya Mpiga Kura wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi Bi. Giveness Aswile akizungumza wakati wa mkutano wa Tume na Wadau wa Uchaguzi Mkoa wa Shinyanga
Mkurugenzi wa Kitengo cha Huduma za Kisheria wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Bw. Seleman Mtibora akiwasilisha mada kwa niaba ya Mkurugenzi wa Uchaguzi mkoani Shinyanga.
Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi Mhe. Balozi Omar Mapuri akizungumza wakati wa mkutano huo
Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi Dkt. Zakia Abubakar akizungumza wakati wa mkutano huo

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post