Dereva,Utingo na abiria wamefariki dunia kwa kuteketea kwa moto huku wengine watatu wakijeruhiwa katika ajali iliyohusisha Malori mawili kugongana uso kwa uso katika eneo la Manzese wilayani Kahama mkoani Shinyanga huku chanzo cha ajali hiyo kikitajwa kuwa uzembe na Mwendokasi.
Inaelezwa kuwa ajali hiyo imehusiha malori mawili ya mizigo ambapo baada ya kugonga uso kwa uso yalianza kuwaka moto na kusababisha vifo vya dereva, utingo na mtu mwingine ambaye anaidawa kuwa ni abiria ambapo jina lake bado halijafahamika.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Shinyanga SACP Janeth Magomi amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo ambayo imehusisha Malori mawili ya Mizigo Namba T 854 DBY lenye tela namba T 180 DVH na Lori namba T 195 EEY lenye tela namba T 811 DYU. #Malunde 1 blog Updates
Social Plugin