Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

LIUNDI : 50/50 TUNAANZA NAYO KWENYE UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 2024

Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP, Bi. Lilian Liundi

Na Mwandishi wetu - Malunde 1 blog

Imeelezwa kuwa ili kufikia usawa wa kijinsia kwa 50/50 ni vyema wanawake wakajitokeza kwa wingi kugombea nafasi za uongozi kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 27,2024.

Rai hiyo imetolewa leo Jumanne Agosti 27,2024 na Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) bi. Lilian Liundi  wakati wa Mdahalo wa Wazi ukiongozwa na Mada 'Ni yapi mafanikio yetu kwa miaka 30+ ya Beijing' kwenye Tamasha la 7 la Jinsia ngazi ya Wilaya 2024 linalofanyika katika Viwanja vya Sabasaba, Wilaya ya Kondoa, Mkoani Dodoma.

"50/50 inawezekana, 50/50 tunaanza nayo kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka huu. Wanawake jitokezeni kugombea nafasi za uongozi, kwani wanawake na wanaume wanapokuwa sehemu moja inaleta tija. Tanzania tunayoitaka ni wanawake kushiriki katika nafasi za uongozi",amesema Liundi.

Katika hatua nyingine Liundi amewataka wanawake na wadau kuendelea kutoa maoni ya Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050 huku akiweka msisitizo kipaumbele kwa masuala ya kijinsia yaingie.

Tamasha la 7 la Jinsia ngazi ya Wilaya 2024 linaloongozwa mada kuu ‘Dira Jumuishi ya 2050: Miaka 30 Baada ya Beijing Tujipange’ limeandaliwa na TGNP kwa kushirikiana na mashirika yanayotetea haki za wanawake na usawa wa jinsia nchini. 

Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP, Bi. Lilian Liundi akielezea kuhusu Mchakato wa Beijing na Maazimio yake wakati wa Mdahalo wa Wazi ukiongozwa na Mada 'Ni yapi mafanikio yetu kwa miaka 30+ ya Beijing kwenye Tamasha la 7 la Jinsia ngazi ya Wilaya 2024 linalofanyika katika Viwanja vya Sabasaba, Wilaya ya Kondoa, Mkoani Dodoma- Picha na Malunde Media
Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP, Bi. Lilian Liundi akielezea kuhusu Mchakato wa Beijing na Maazimio yake wakati wa Mdahalo wa Wazi ukiongozwa na Mada 'Ni yapi mafanikio yetu kwa miaka 30+ ya Beijing kwenye Tamasha la 7 la Jinsia ngazi ya Wilaya 2024 linalofanyika katika Viwanja vya Sabasaba, Wilaya ya Kondoa, Mkoani Dodoma
Mwanaharakati Happy Maruchu akielezea  Changamoto za utekelezaji wa maazimio ya Beijing na masuala ya ukatili wa kijinsia yanaibuka katika utekelezwaji wa maazimio ya Beijing kwa Tanzania wakati wa Mdahalo wa Wazi ukiongozwa na Mada 'Ni yapi mafanikio yetu kwa miaka 30+ ya Beijing kwenye Tamasha la 7 la Jinsia ngazi ya Wilaya 2024 linalofanyika katika Viwanja vya Sabasaba, Wilaya ya Kondoa, Mkoani Dodoma
Mwanaharakati Happy Maruchu akielezea  Changamoto za utekelezaji wa maazimio ya Beijing na masuala ya ukatili wa kijinsia yanaibuka katika utekelezwaji wa maazimio ya Beijing kwa Tanzania
Mwanaharakati Happy Maruchu akielezea  Changamoto za utekelezaji wa maazimio ya Beijing na masuala ya ukatili wa kijinsia yanaibuka katika utekelezwaji wa maazimio ya Beijing kwa Tanzania
Mwanaharakati Agness Lukanga akielezea  Utekelezwaji wa Maazimio ya Beijing kwa Tanzania wakati wa Mdahalo wa Wazi ukiongozwa na Mada 'Ni yapi mafanikio yetu kwa miaka 30+ ya Beijing kwenye Tamasha la 7 la Jinsia ngazi ya Wilaya 2024 linalofanyika katika Viwanja vya Sabasaba, Wilaya ya Kondoa, Mkoani Dodoma

Mwenyekiti wa Bodi ya Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Gemma Akilimali akichangia hoja wakati wa Mdahalo wa Wazi ukiongozwa na Mada 'Ni yapi mafanikio yetu kwa miaka 30+ ya Beijing kwenye Tamasha la 7 la Jinsia ngazi ya Wilaya 2024
 Flora Ndaba Muongozaji Mdahalo wa Wazi ukiongozwa na Mada 'Ni yapi mafanikio yetu kwa miaka 30+ ya Beijing kwenye Tamasha la 7 la Jinsia ngazi ya Wilaya 2024 akizungumza wakati Tamasha la 7 la Jinsia ngazi ya Wilaya 2024 linalofanyika katika Viwanja vya Sabasaba, Wilaya ya Kondoa, Mkoani Dodoma

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com