Na Paul Kayanda,Kahama
Mwenyekiti wa Taasisi ya Mzalendo Foundation na aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga, Hamis Mgeja, ameungana na familia ya mwandishi mwandamizi wa habari, Mohab Dominick, katika maziko ya mama yake mzazi, Tekra Limi, aliyefariki dunia akiwa na umri wa miaka 91.
Maziko hayo yalifanyikaAgosti 27,2024 katika makaburi ya Kanisa Katoliki Mbulu, katika Manispaa ya Kahama, mkoani Shinyanga. Viongozi mbalimbali wa chama na serikali walihudhuria tukio hilo, wakitoa heshima zao za mwisho kwa marehemu na pole kwa familia iliyoachwa.
Akizungumza katika maziko hayo, Mgeja alitoa neno la faraja kwa familia ya Mohab Dominick, akiwatia moyo kuwa Bwana ametoa na Bwana ametwaa, jina lake lihimidiwe.Alisema kuwa ingawa ni kipindi kigumu, wanapaswa kuwa na imani na kumshukuru Mungu kwa kila jambo.
Maziko hayo yameacha simanzi kubwa kwa familia, marafiki, na wale wote waliomfahamu marehemu Tekra Limi, ambaye alijulikana kwa upendo wake na huruma kwa wengine na aliyetumika katika chama na serikali na muasisi wa Tanu yapo mengi mama amewaachia wanasiasa na liwe la kujifunza.
Social Plugin