Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

CHUO CHA KIJESHI-CSC -CHATOA TUZO KWA KIWANDA CHA MATI SUPER BRAND LTD


Na Jaliwason Jasson, MANYARA

CHUO cha kijeshi Command and staff college cha Tanzania (CSC) kimetoa Tuzo Maalum kwa Kiwanda cha Mati Super Brands Limited ili kutambua mchango wake katika kuifikia jamii.

Akizungumzia Tuzo hiyo maalum Mkurugenzi Mtendaji wa Mati Super Brands Limited David Mulokozi leo Agosti 31,2024  amesema tuzo hiyo itawaongezea molali ya kufanya kazi na ndio Tuzo kubwa ya pili tokea wameanza kupata Tuzo ambapo miongoni mwa Tuzo kubwa walizowahi kupata kubwa ni waliyopewa na Rais Samia Suluhu Hassan mwaka jana.

Mulokozi amesema chuo hicho kimewapatia tuzo maalum kutokana na kutambua mchango wao ambao wanautoa katika jamii katika maeneo ya mazingira, Afya, elimu, upandaji miti na jamii.

Aidha amesema chuo hicho kimekuwa ni wadau na wabia kwa muda mrefu na wamekuwa wakiwaletea wanafunzi kuja kujifunza kutoka mataifa tofauti katika usalama wa chakula na uzalishaji.
Mulokozi amewaondoa hofu watu waliosomea nje wanaoogopa kuja kuwekeza hapa nchini.

"Soko la Tanzania lipo watu waje wawekeze nchi yetu ni salama utaweka mtaji wako utakuwa salama na kufanya biashara,"alisema Mulokozi

Amesema mazingira ya biashara ni mazuri serikali imeweka sera nzuri kuna mabadiliko ya sera kila baada ya miaka mitatu.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com