Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Yusuph Mwenda akizungumza na wafanyabiashara mkoa wa Shinyanga Agosti 15,2024
Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Yusuph Mwenda amesema Mamlaka hiyo imedhamiria kuimarisha zaidi ushirikiano baina yake na Wafanyabiashara nchini akisisitiza TRA haipo kwa ajili kufunga biashara zao bali kurahisisha biashara.
Mwenda ametoa kauli hiyo leo Alhamisi Agosti 15,2024 alipokutana na kufanya mazungumzo na wafanyabiashara mkoa wa Shinyanga kwenye kikao kilichofanyika katika ukumbi wa Vigirmark Hotel Mjini Shinyanga chenye lengo la kupokea maoni ya wafanyabiashara.
“TRA ipo kwa ajili ya kurahisisha shughuli za kiuchumi siyo kuua biashara. TRA inataka kurahisisha kazi zenu wafanyabiashara. TRA ni chombo chenu, TRA haipo kufunga biashara zenu, ipo kurahisisha Tunataka kuona biashara zinafunguliwa, tutafanya kila namna kuhakikisha baishara hazifi. Haya yote yanawezekana tukiwa na ushirikiano kati yetu”,amesema Mwenda.
Katika hatua nyingine Mwenda amesema TRA itachukua hatua bila kumpendelea wala kumuonea yeyote atakayehusika kukwepa kodi au kwa Afisa atakayeonesha kukosa uadilifu kwenye majukumu yake
"Hatutakuwa na huruma kwa wanaokwepa kodi, hao wanaokwepa kodi waache kufanya hivyo kwani hizo pesa ni za watanzania. Toeni taarifa za wanaokwepa kodi. Pia mnapodaiwa kodi msikimbie, njooni TRA tuzungumze, mtashauriwa namna ya kulipa kodi",ameongeza Mwenda.
"Mimi nimekutana na nyinyi, meneja wa Mkoa atakutana na nyinyi na viongozi wengine wataendelea kukutana nanyi, Naahidi tutawahudumia vizuri, naomba muwe mabalozi wa TRA tumieni App yetu kutoa maoni, Mameneja wa mikoa na wilaya ni lazima wawasikilize walipa kodi",amesema.
Aidha amewashukuru Wafanyabiashara mkoani Shinyanga kwa kuendelea kuwa walipa kodi wazuri ambapo kwa mwaka wa fedha uliopita Shinyanga imekuwa mkoa Kinara kwa ulipaji kodi nchini .
"Mwaka huu wa fedha TRA tunataka kukusanya kodi shilingi Trilioni 30.4, na kodi hizi tutazikusanya pamoja.. Na Shinyanga ni sehemu tunayoitegemea. Kwa TRA Shinyanga ni kubwa, kuna walipa kodi wakubwa ukiwemo mgodi wa Almasi wa Williamson Diamond Ltd",amesema.
Nao wafanyabiashara Mkoani Shinyanga wameipongeza TRA kwa utaratibu huo wa kukutana na wafanyabiashara na kusikiliza changamoto zinazowakabili na kwamba mikutano hiyo inafanya wajiamini.
Pia wameiomba TRA kuboresha zaidi mazingira ya ulipaji kodi ili waendelee kulipa kodi kwa hiari huku wakiomba ukusanyaji wa madeni ya nyuma (malimbikizo ya nyuma) upotezewe, kuwe na kodi rafiki huku wakilalamika kuhusu VAT, Service levy, kodi nyingi kuwekwa kwenye kapu moja na wachimbaji wadogo kutozwa kodi kubwa na baadhi ya wafanyabiashara kufungiwa akaunti zao za benki bila taarifa.
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Yusuph Mwenda akizungumza na wafanyabiashara mkoa wa Shinyanga Agosti 15,2024 - Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Yusuph Mwenda akizungumza na wafanyabiashara mkoa wa Shinyanga Agosti 15,2024
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Yusuph Mwenda akizungumza na wafanyabiashara mkoa wa Shinyanga Agosti 15,2024
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Yusuph Mwenda akizungumza na wafanyabiashara mkoa wa Shinyanga Agosti 15,2024
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Yusuph Mwenda akizungumza na wafanyabiashara mkoa wa Shinyanga Agosti 15,2024
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Yusuph Mwenda akizungumza na wafanyabiashara mkoa wa Shinyanga Agosti 15,2024
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Yusuph Mwenda akizungumza na wafanyabiashara mkoa wa Shinyanga Agosti 15,2024
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Yusuph Mwenda akizungumza na wafanyabiashara mkoa wa Shinyanga Agosti 15,2024
Naibu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mcha Hassan Mcha akizungumza kwenye mkutano huo
Naibu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mcha Hassan Mcha akizungumza kwenye mkutano huo
Kamishna wa Walipa Kodi Wakubwa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Michael Mhoja akizungumza kwenye mkutano huo
Kamishna wa Walipa Kodi Wakubwa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ,Michael Mhoja akizungumza kwenye mkutano huo
Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Shinyanga, Josephat Mwaipaja akizungumza kwenye mkutano huo
Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Shinyanga, Josephat Mwaipaya akizungumza kwenye mkutano huo
Mwenyekiti wa TCCIA Mkoa wa Shinyanga, Jonathan Manyama Kifunda akizungumza kwenye mkutano huo
Social Plugin