YANGA HII UNAIFUNGAJE? UTABIRI WA DR. MANGURUWE WATIMIA

Yanga SC wametumia dakika 44 kuwaadhibu Simba katika Ngao ya Jamii mchezo wa nusu fainali Uwanja wa Mkapa Jijini Dar es salaam!


YANGA hii unaifungaje? Mashabiki wametuma tambo kimtindo kwa watani zao wa jadi baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 kwenye mchezo wa hatua ya nusu fainali Ngao ya Jamii, Uwanja wa Mkapa.

Ngoma imemalizwa dakika 44 za kipindi cha kwanza baada ya Simba kufanya makosa kwenye kuokoa mpira ambao ulionekana hauna madhara kwenye miguu ya Pacome Zouzoa ambaye alimpa pasi Prince Dube aliyemuachia Maxi Nzengeli.

Nzengeli ambaye alikuwa kwenye ubora wake alimtungua Kipa mpya wa Simba Moussa ambaye ameonekana kuwa kwenye ubora wake katika mchezo licha ya kufungwa.

Mwamuzi wa kati Elly Sassi alifanya kazi yake kupeleka mpira kati mara moja ikiwa ni kipindi cha kwanza na mpaka dakika 45 zinagota mwisho ngoma ilikuwa ni Yanga 1-0 Simba.

Fainali ni Agosti 11 2024 Yanga v Azam FC huku Simba ikicheza mchezo wa hatua ya kusaka mshindi wa tatu dhidi ya Coastal Union ya Tanga.


UTABIRI WA DR. MANGURUWE UMETIMIA

DR MANGURUWE alitabiri matokeo ya Derby ya Kariakoo leo, ambapo alitabiri kuwa Simba Sc anaenda kufungwa na Mtani wake Yanga Sc kwenye Mchezo wa leo pale Mkapa Stadium japokuwa Dr Manguruwe yeye mwenyewe  ni shabiki kindakindaki wa Simba Sc. 

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post