Na Marco Maduhu,SHINYANGA
TIMU ya Masekeo wameibuka na ushindi katika fainali ya Dr. Samia /Katambi Cup, kwa kuichapa timu ya Ngokolo kwa mikwaju ya Penati 9 kwa 8.
Fainali hiyo imechezwa leo Agosti 31,2024 katika viwanja vya Chuo cha Ualimu Shinyanga (SHYCOM)huku Mgeni Rasmi akiwa ni Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)Mkoa wa Shinyanga Mabala Mlolwa.
Katika mechi hiyo ya fainali timu ya Masekelo ilianza kufunga bao la kwanza na kisha kusawazishiwa, na hadi kipenga kinapulizwa dakika 90 timu zote zilitoka na bao moja moja, wakaenda kwenye mikwaju ya penati.
Aidha, Penati zilipigwa tano tano zikaishi huku hakuna aliyekosa goli kisha zikaanza kupigwa moja moja ndipo timu ya Masekelo wakapata penati 9 kwa 8 na kuibuka washindi kwenye michuano ya Dr.Samia/Katambi Cup ambayo ilishirikisha timu 32.
Michuano hiyo ya Dr.Samia Katambi Cup Mshidi wa kwanza ambaye ni Masekelo ameibuka na kitita cha Sh.milioni 6, kombe, Jezi pamoja na medali, na mshidi wa pili ambaye ni Ngokolo amepata Sh.milioni 3 Jezi na Medali, na Mshindi wa tatu ambaye ni Kashwasa amepata Sh.milioni moja, jezi na medali.
Pia mfungaji bora katika michuano hiyo aliibuka ni Izack Eliota ambaye alipata kiatu cha dhahabu,huku kipa bora akiibuka Laurent kutoka Ndembezi naye alipata zawadi, pamoja na wachezi waliofunga hat trick nao walipata zawadi ya mipira kila mmoja.
Kwa timu ambao ziliingia Robo fainali nazo zilipata jezi za mipira.
Awali Mgeni Rasmi Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga Mabala Mlolwa, akizungumza wakati wa ufunguzi wa fainali hiyo, amempongeza Mbunge Katambi, kwamba amemheshimisha Rais Samia Suluhu Hassan kwa kumpatia jina lake kwenye mashindano hayo, na pia Rais ni mpenda michezo na amemuunga mkono kwa vitendo.
Amesema ligi hiyo imeibua vipaji vingi vya vijana na watapata ajira kupitia ligi hiyo, sababu mchezo kwa sasa ni ajira na vijana wengi wamepata ajira kupitia michezo.
TAZAMA PICHA HAPA CHINI👇👇
Mfungaji bora katika michuano hiyo Izack Eliota ambaye alipata kiatu cha dhahabu.
Goli kipa bora Laurent akipa zawadi.
Timu ya Masekelo akipewa kombe lao baada ya kuibuka washindi.
Timu ya Masekelo akipewa kombe lao baada ya kuibuka washindi.
Timu ya Masekelo akipewa kombe lao baada ya kuibuka washindi.
Timu ya Masekelo akipewa kitita cha Sh.milioni 6 baada ya kuibuka washindi.
Timu ya Masekelo akipewa kitita cha Sh.milioni 6 baada ya kuibuka washindi.
Zawadi zikiendelea kutolewa kwa washindi wa pili timu ya Ngokolo Sh.milioni 3.
Washindi wa tatu Kashwasa wakipewa sh.milioni moja.
Zawadi zikiendelea kutolewa .
Waamuzi wakipewa Medali.
Wachezaji wa Masekelo wakivalishwa Medali.
Awali Viongozi wakiwa meza kuu wakiangalia soka.
Mikwaju ya penati ikiendelea kupigwa.
Wananchi wakiangalia soka.