Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

BUNGE KUTUMIA BONANZA KUDUMISHA MAHUSIANO NA TAASISI NYINGINE



Na Dotto Kwilasa, Dodoma

Benk ya NMB kwa kushirikiana na Bunge Bonanza wanatarajia kufanya bonanza ambalo ni muendelezo wa mabonanza yote yaliopita.

Mwenyekiti wa Bunge Bonanza na Bunge Marathon Festo Sanga ameeleza hayo leo Agosti 29 ,2024 Jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari wakati akipokea vifaa vya michezo ya bonanza hilo.

Mwenyekiti huyo amesema bonanza hilo litafanyika tarehe 31 Katika viwanja vya Johnmerline huku akibainisha bonanza hilo linakusudia kuleta hamasa na mahusiano na taasisi zingine.

" Kama Spika wetu wa bunge alivyoagiza Bunge tujenge mahusiano mazuri na taasisi hivyo bonanza hili linakwenda kidumisha mahusiano mema, " Amesema Mwenyekiti Sanga

Sanga amesema,"Bonanza hilo linakwenda kuunga mkono juhudi za Viongozi wa juu wa serikali za kutaka jamii kufanya mazoezi ili kuondokana na magonjwa yasiyo ya lazima ambayo yamekuwa yakiigharimu serikali kutibu wananchi, "ameeleza

Amesema watatumia bonanza hilo kuhamasisha watu kushiriki katika zoezi la uchaguzi mkubwa 2025 na uchaguzi mdogo wa serikali za mitaa Mwaka huu, huku akibainisha kuwa bonanza hilo litakuwa na michezo tofauti tofauti ambapo wabunge na wafanyakazi wa taasisi zingine watashiriki michezo hiyo.

Kwa Upande wake Meneja NMB Kanda ya Kati Janeth Shango amelishukuru Bunge la Tanzania kulidhia kushiriki bonanza hilo ni wazi kuwa Benk ya NMB tunakubarika.

" Niwaombe tu wabunge mfanye mazoezi ya nguvu kwani Sisi kama Benk ya NMB tunakuja kushindana na hitani letu ni kushinda,kauli mbiu katika bonanza hili ni "Shiriki Uchaguzi kwa maendeleo ya nchi yetu"amefafanua

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com