DC MOYO ATEMBELEA BANDA LA TBS MAONESHO NANENANE LINDI


MKUU wa Wilaya ya Nachingwea, Mohammed Moyo amewaasa wajasiriamali kuhakikisha wanazalisha bidhaa zilizo bora na kuweza kusajili na Shirika la Viwango Tanzania ili kupata alama ya ubora kwenye bidhaa zao.

Wito huo ameutoa leo Agosti 7,2024 kwenye Maonesho ya Nanenane yanayofanyika katika Viwanja vya Ngongo mkoani Lindi.

Aidha amewataka wazalishaji na wasambazaji wa bidhaa kuendelea kuzalisha na kuuza bidhaa zenye ubora na zinazotambuliwa na kupitishwa na Shirika la Viwango ili kuhakikisha wanalinda usalama wa afya za wananchi kwa ujumla.

Kwa upande wake Meneja wa TBS Kanda ya Kusini, Mhandisi Said Mkwawa amesema katika maonesho hayo TBS inakutana na wajasiriamali na kuwahamasisha namna watakavyoweza kuzalisha bidhaa zenye ubora zikapata alama ya ubora na kuuzwa nje ya nchi.

Amesema Serikali imekuwa ikitoa fedha kwaajili ya wajasirimali ambapo TBS wanakwenda kumkagua mjasiriamali bure ikiwemo kupima bidhaa maabara ambalo jukumu hilo hufanywa na TBS bila malipo.

Aidha Mhandisi Mkwawa ametoa rai kwa wajasiriamali kujitahidi kuzalisha bidhaa ambazo zinakidhi matakwa ya viwango ili kulinda afya ya watumiaji wa bidhaa. hizo na kuepuka kuzalisha bidhaa zilizo chini ya viwango kwani zinahatarisha afya,uchumi na usalama.

"Shirika la Viwango haturuhusu iwe kuzalisha au kuingiza nchini bidhaa zote zenye viwango hafifu kwani zitaleta athari kiuchumi,kiafya na kiusalama kwa ujumla" amesema Mhandisi Mkwawa

Pamoja na hayo ameeleza kuwaTBS imekuwa na utaratibu wa kufanya kaguzi mara kwa mara kwenye maeneo ya uzalishaji ili kubaini makubaliano yao na mzalishaji kama bado yanazingatiwa. kwa lengo la kuhakikisha usalama kwa watumiaji wa bidhaa hizo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post