Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

DKT. BITEKO AHIMIZA WANANCHI KUSHIRIKI UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA








Na Dotto Kwilasa, Dodoma

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko ametoa rai kwa Watanzania kuchagua Viongozi wa Serikali za Mitaa wanaofaa kwa maendeleo ya Taifa.
Dkt. Biteko amesema hayo leo Agosti 31, 2024 wakati wa NMB Bunge bonanza iliyofanyika katika viwanja vya Shule ya John Merlin jijini Dodoma.

Amesema Tanzania inahitaji viongozi wenye maono na mapenzi na nchi hivyo ni jukumu la kila mtanzania kujiandaa kushiriki kikamilifu kwenye uchaguzi.

Akizungumzia bonanza hilo Dk. Biteko amesema hamasa kwa watanzania kuendelea kuchangia maendeleo huku akitumia nafasi hiyo kutoa rai kwa jamii kiendeleza utamaduni wa kufanya mazoezi kwa afya.

Kwa upande wake Spika wa Bunge Tulia Ackson amesema bonanza hilo litasaidia kuchangia ujenzi shule ya wavulana Bunge.

Amesema hatua hiyo itasaida kuleta usawa kwa watoto wote wa kiume na wa kike.

"Tulianza na shule ya sekondari ya wasichana na sasa Bunge linaenda kufanya hivyo hivyo kwa wavulana, tunahitaji kuwalea watoto wote kwa usawa kila mtoto ni muhimu, " amesisitiza

Pamoja na Mambo mengine bonanza hilo limeandaliwa na Benki ya NMB ambayo imetoa jumla ya shilingi milioni 50 kama mchango wa ujenzi wa shule ya wavulana ikiwa ni shukurani kwa jamii.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com