DKT. MPANGO AILEKEZA WIZARA YA MADINI KUSIMAMIA MADINI MKAKATI KWA MANUFAA YA WATANZANIA






Na mwandishi wetu, Dodoma

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango ameitaka Wizara ya Madini kuhakisha inasimamia vyema uvunaji wa madini ya kimkakati ili nchi iweze kunufaika nayo.

Dkt. Mpango ameyasema hayo leo Katika eneo la Mpwayungu, Wilaya ya Chamwino-Dodoma wakati akihitimisha ziara ya siku 4 ya Mkoa wa Dodoma.

“Mwenyezi Mungu ametujaalia rasilimali hii ya madini mkakati yenye mahitaji makubwa sana Duniani," amesema Dkt. Mpango.

Amesema Mkoa wa Dodoma umebarikiwa kuwa na madini mkakati kwa wingi na aina tofauti tofauti, na kueleza kuwa ni lazima rasilimali hiyo ikatafsirike katika maendeleo ya wananchi wa Dodoma na Tanzania kwa ujumla.

"Wizara ya Madini hakikisheni mnaweka mpango mzuri wa usimamizi wa rasilimali hii kwa manufaa ya Taifa na kwa manufaa ya vizazi vijavyo” amesema Dkt. Mpango.

Akiwasilisha salamu za Wizara Waziri wa Madini Mhe Anthony Mavunde amemwahidi Dkt.Mpango kuyafanyia kazi maelekezo yote na kwasasa Wizara inakamilisha andiko la mkakati wa usimamizi na uvunaji wa madini hayo ili yalete faida kwa nchi kwa kuchochea uchumi na kuendeleza sekta ya madini.

Mhe. Mavunde ametumia fursa hiyo kutoa maelekezo kwa Maafisa Madini Wakazi kuhakikisha wanasimamia ipasavyo maeneo yenye uchimbaji wa madini mkakati ili manufaa yake yaonekane kwa Taifa.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post