|
|
Na Oscar Assenga, TANGA
SHIRIKA la Madini la Taifa (Stamico) limesema
kwamba agenda yao katika kutunza mazingira sio kupanda miti na kuiacha bali ni
kuhakikisha wanaisimamia katika ukuaji wake mpaka inapokuwa mikubwa.
Kauli hiyo ilitolewa leo na Mkurugenzi wa wa
Shirika la Taifa la Madini Tanzania (STAMICO) Dkt Venance Mwase wakati
akishiriki zoezi la upandaji wa miti katika eneo la Amboni Jijini Tanga lililoratibiwa
na Wanawake na Samia Mkoa wa Tanga lililokwenda sambamba na kutambulisha
Nishati Safi mbadala ya Rafiki
Briquettes.
Alisema katika agenda hiyo wanazuia pia kukata
miti na ili kuizuia lazima kuwa na nishati safi mbadala ya Rafiki Briquettes ambao
ni ubunifu uliofanya na shirika hilo katika kuhakikisha suala la utunzaji wa
mazingira linapewa umuhimu mkubwa
“Lakini suala la nishati safi ya kupikia ni
agenda ya Rais hivyo niwapongeza wanawake na Samia mkoa wa Tanga kwa kuunga
mkono agenda hiyo hivyo tutaendelela kuwaunga mkono “Alisema
Aidha alisema kwamba wanawajibu wa kutunza mazingira
na kufanya hivyo lazima waangalie nini kinafanya mazingira yanaharibika
wananchi wengi bado hawana nishati mbadaa bado wanatumia kuni na mkaa ambao
unatokana na miti hali ambayo inawafanya kwenda kukata miti ili kupata nishati
ya kupikia.
Alisema kwamba programu yao hiyo inakwenda na
vitu viwili kwanza hiyo miti inayokatwa wanataka wahamasishe ili ipandwa ndio
kitu wanachokifanya ili kuzuia isikatwe
wananchi lazima apike na ale ndio maana wamekuja hiyo nishati mbadala ya
kupikia ya Rafiki inatokana na ubunifu na utafiti uliofanywa na shirika la
madini la Taifa (Stamico) .
Alisema ili kuhakikisha wanapata nishati
mbadala kwa ajili ya wananchi ambayo ni
rafiki kwa matumizi,mazingira na bei kutokana na vipato vyao kwa hiyo
wameitamblisha hiyo bidhaa mkoani Tanga .
“Kimsingi utafiti umekamilika na uzalishaji
umeanza na namna ya kuuza hiyo bidhaa kundi la wanawake na samia ndio watakuwa
wauzaji watakuwa wanazalisha viwandani na watakauokuwa wanaiuza na kuhamasisha
matumizi hayo watakuwa ni wakina mama
kwa sababu wanakina mama ndio wanaathirika zaidi na utafutaji wa nishati
na uchafuzu wa mazingira maana wanasema uchungu wa mwana ni mzazi”Alisema
Alisema kwamba ndio sababu ya kuwapa fursa
hiyo ili waunge mkono agenda ya Rais ya mazingira na nishati mbadala ya kupikia
lakini hiyo bidhaa impe uchumi huku akieleza kwa kuisambazaji haitakuwa kazi ya
bure ni ya kibiashara na watawawesha kuwa na kontena na eneo la kuuzia na kuwatangazia
na kwenye matukio mbalimbali kama hayo watawasaidia ili kuhakikisha wameweka
hamasa kwa wananchi wote waache na kukuata miti na watumie nishati safi mbadala.
“Agenda ya mazingira ni ya Rais hivyo
mmeichagua jambo sahihi kwa wakati sahihi tutawasapoti tunatunza mazingiwa kwa
vizazi vya sasa na vijavyo na mazingira yamekwenda kwenye kuingia kwenye ajira
ya uchumi “Alisema
Hata hivyo alisema mazingira yanapochafuliwa
yatakuja kuathiri baadae na watashindwa kulima, kupata hewa nzuri huku
akiwataka kulifanya zoezi hilo liwe endelevu na wanapopanda miti lazima waitunze.
Awali akizungumza katika zoezi hilo
Mwakilishi wa wanawake na Samia walimshukuru Dkt Mwase kwa kuja Tanga kuungana
nao katika zoezi hilo kutokana na kwamba wanawake na samia wapo mikoa 25 hapaa
nchini lakini ameweza kuitika kuwa pamoja.
“Kwa pamoja huo ni muendelezo wamepanda miti
leo ili waweze kutumia mkaa mbadala hivyo wanawake na samia wana deni la kwenda
kuhamasisha wananchi jinsi gani ya kuacha kukata miti na kutumia kuni katika
kupika na kueleza athari zake kwa kutoa
elimu kwa wananchi ili fursa inapokuwa imekamilika wawe na uelewa wa pamoja”Alisema
Naye kwa upande wake Mwakilishi wa Mkurugenzi
wa Bonde la Mto Pangani Michael Buli alisema kwamba katika kampeni hiyo ya wanawake
na samia mkoa wa Tanga ya kutunza mazingira watakuwa nao bega kwa bega
kushirikiana katika kutunza mazingira na
vyanzo vya maji katika maeneo yote yanayostahili.
Michael ambaye ni katibu wa Jumuiya ya watumiaji Maji wa Bonde Zigi chinialisema kqa sababu mazingira yamekuwa hatarishi sana na wakiendelea hivyo miaka 10 ijayo Tanzania itaendelea kuwa ya kijani na kama watakuwa nyuma basi Tanzania itakuwa nyeusi .
Social Plugin