I & M BANK WAJA NA HUDUMA KWA WHATSAPP

 

Mtendaji Mkuu wa Benk ya I&M Zahid Mustafa akizungumza leo na wanahabari jijini Dar es salaam wakati wa uzinduzi wa huduma ya kisasa ya Rafiki Chat Bankin iliyoboreshwa inapatikana kupitia WhatsApp.

Mtendaji Mkuu wa Benk ya I&M Zahid Mustafa (kushoto) akiwa na Zainabu Maalim (kulia) ambaye ni Mkuu wa Kitengo kwa wateja wa Benk ya I&M wakati wakizungumza leo na na wanahabari jijini Dar es salaam wakati wa uzinduzi wa huduma ya kisasa ya Rafiki Chat Bankin iliyoboreshwa inapatikana kupitia WhatsApp.
Mkuu wa Kitengo cha wateja Rejareja Benk ya I&M Simon Gachachi akizungumza leo na wanahabari jijini Dar es salaam wakati wa uzinduzi wa huduma ya kisasa ya Rafiki Chat Bankin iliyoboreshwa inapatikana kupitia WhatsApp.
Meneja wa bidhaa za kidijitali wa Benk ya I&M Adam Emmanue Adam Emmanuel akielezea manufaa ya huduma hiyo katika mkutano leo na wanahabari jijini Dar es salaam wakati wa uzinduzi wa huduma ya kisasa ya Rafiki Chat Bankin iliyoboreshwa inapatikana kupitia WhatsApp.
Mkuu wa Kitengo kwa wateja wa Benk ya I&M Zainabu Maalimu akizungumza leo na wanahabari jijini Dar es salaam wakati wa uzinduzi wa huduma ya kisasa ya Rafiki Chat Bankin iliyoboreshwa inapatikana kupitia WhatsApp.
Meneja wa bidhaa za kidijitali wa Benk ya I&M Adam Emmanue Adam Emmanuel akielezea namna ya kujisajili katika huduma hiyo mbele ya wanahabari jijini Dar es salaam wakati wa uzinduzi wa huduma ya kisasa ya Rafiki Chat Bankin iliyoboreshwa inapatikana kupitia WhatsApp.
Meneja wa uendeshaji huduma za kidigitali Ojugu Laizer akizungumza leo na wanahabari jijini Dar es salaam wakati wa uzinduzi wa huduma ya kisasa ya Rafiki Chat Bankin iliyoboreshwa inapatikana kupitia WhatsApp (na Mussa Khalid)

............................

NA MUSSA KHALID 

 Benki ya I&M imeanzisha huduma ya kisasa ya Rafiki Chat Banking iliyoboreshwa ili kuwarahisishia huduma wateja wao. 

Imeelezwa kuwa huduma hiyo ambayo inapatikana kupitia WhatsApp inatoa huduma mbalimbali za kibenki ikiwa ni pamoja na kuangalia salio la akaunti papo kwa papo, kupokea taarifa za miamala pamoja na kuhamisha au kutuma fedha kirahisi. 

Akizungumza jijini Dar es salaam wakati wa uzinduzi huo Mtendaji Mkuu wa Benki hiyo Zahid Mustafa amesema benki hiyo inaendelea kufanya ubunifu kwa mustakabali endelevu na kuunga mkono ubadilishaji wa kigijitali nchini. 

“Sisi kama I&M sio tu kwamba hii ni bidhaa yetu ya kwanza bali tupo tunajikita zaidi kwenye dhamira kuingia kwenye ulimwengu wa kidijitali lakini pia tumeingia ushirikiano na Airtel inaitwa kamilisha ambapo tunaweza kuwafikia watanzani wengi zaidi na kuwapa huduma bora zaid’amesema Mustafa 

Kwa upande wake Mkuu wa Kitengo cha wateja Rejareja katika benki hiyo Simon Gachachi amesema kuwa malengo yao wanakusudia kuwekeza katika kujenga utendaji zaidi na vipengele vinavyofanya kazi kwa washirika wao wa teknolojia. 

Aidha amesema kuwa katika huduma hiyo pia mwezi septemba watazindua namna mteja ataweza kulipa kodi na malipo mengine ya serikali kupitia WhatsApp kwa kutumia mifumo mbalimbali. 

Amesema wameshirikiana serikali ambapo imechukua kipaumbele kusaidia benki kuendelea kufanya uwekezaji katika teknolojia ya ubunifu. 

Akizungumzia huduma hiyo Meneja wa bidhaa za kidijitali wa benki hiyo Adam Emmanuel amesema kuwa huduma hiyo walianzisha tangu mwaka 2021 ambapo wamefanya maboreso mbalimbali ikiwemo kuwaruhusu wateja wapya kujisajili na kufungua akaunti.

Amesema kuwa vipengele vilivyoboreshwa ni pamoja na uwezo wa kujisajili mwenyewe unaotumia teknolojia ya AI,muonekano ulioboreshwa kwa mtumiaji,usaidizi wa wateja kwa msaada wa AI,na sehemu ya maswali na majibu yanayoulizwa mara kwa mara.

“Mchakato wa usajili ni rahisi tu ambapo ni sevu namba ya WhatsApp Banking iliyothibitishwa ya I&M Banki +255 755 674696 kisha tuma neno habari halafu fuata maelekezo", amesema Adam

Zainabu Maalimu ni Mkuu wa Kitengo kwa wateja amesema hayo yote yanajiri kutokana na kutimiza miaka 50 ya benki hiyo kwa mwaka huu hivyo wametambua muelekeo wa dunia katika matumizi ya mitandao katika kufanya shughuli mbalimbali.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post