ILEMELA YAPONGEZWA KWA KUTEKELEZA MRADI WA KUPANGA, KUPIMA NA KUMILIKISHA ARIDHI.


Kamati ya kudumu ya Bunge ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa – TAMISEMI ikiongozwa na Mwenyekiti wake Mhe. Justine Nyamoga imeipongeza Halmashauri ya wilaya ya Ilemela kwanamna ambavyo imetekeleza kwa mafanikio makubwa Programu ya Kupanga, Kupima na Kumilikisha Aridhi katika Halmashauri yao.

Kamati imetoa pongenzi hizo katika Kikao cha Kamati cha kupokea Taarifa ya Urejeshaji wa Mikopo ya Kupanga, Kupima na Kumilikisha Aridhi (KKK) unaotekelezwa katika Halmashauri mbalimbali Nchini kwa Fedha zilizotolewa na Wizara ya Aridhi, kilichofanyika katika Ukumbi wa Anna Makinda Bungeni Jijini Dodoma.

Halmashauri ya Wilaya ya Ilemela ilipokea mkopo kutoka wizara ya Aridhi jumla ya Shilingi Bil. 3,589,774,000 ambapo ilifanikiwa kurejesha mkopo wote.

Halmashauri nyingine ambazo zimerejesha Mkopo wote ni Halmashauri za Wilaya ya Moshi, Jiji la Mwanza, Wilaya ya Meru, Morogoro Manispaa, Wilaya ya Kilosa, Wilaya ya Geita, Mji wa Bariadi, Wilaya ya Mbozi, Mji wa Tunduma, Wilaya ya Songwe, Wilaya ya Kaliua, Manspaa ya Kigamboni, Mji wa Kibaha Pamoja na Ofisi ya Aridhi ya Mkoa wa Iringa.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post