Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan,akimkabidhi Tuzo Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Meja Jenerali Rajab Mabele mara baada ya kuibuka Mshindi wa kwanza wa Jumla katika Maonesho ya Nanenane Kitaifa yaliyofanyika viwanja vya Nzunguni Dodoma
Na Alex Sonna-DODOMA
Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Limepata Tuzo ya Ushindi wa kwanza wa Jumla Maonesho ya Nanenane Kitaifa yaliyofanyika viwanja vya Maonesho Nzunguni Dodoma.
Tuzo hiyo imekabidhiwa kwa Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Meja Jenerali Rajab Mabele na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Akiongea na Waandishi wa Habari mara baada ya kupokea tuzo hiyo, Meja Jenerali Mabele amesema kuwa ushindi walioupata katika maonesho hayo yanatokana na utekelezaji wa shughuli hizo kila wakati.
Meja Jenerali Mabele ameongeza kuwa, hakuna ushindi unapotikana bila bidii na kuwa JKT imekuwa ikifanya juhudi katika sekta hizo. “Tulidhamiria kuifanya kazi hii, tulidhamiria kuhakikisha tunashinda, hakuna ushindi unakuja bila bidii, sisi tumeonesha bidii.” Alisema katika maonesho hayo, JKT imeshiriki katika sekta zote za kilimo, mifugo na uvuvi.
Amesema katika kilimo, wamekuwa wakifanya kilimo cha kisasa kupitia mazao ya chakula, biashara na Mazao ya kimkakati ambayo yanatumika kama shamba darasa kuwafundisha Vijana wanaopatiwa Mafunzo ya JKT katika Vikosi vyake vyote.
Amesema pia wamekuwa wakifanya shughuli za ufugaji wa kisasa katika Maonesho hayo ili wananchi waweze kujifunza.
Amesema kwa upande wa uvuvi, JKT imekuwa likifuga n'gombe, Mbuzi, Kuku, Bata nk lakini pia limeanzisha teknolojia ya ufugaji wa samaki kwa njia mbalimbali ikiwemo Vizimba, Matanki ambapo mfugaji anatumia eneo dogo na kupata faida kubwa.
Meja Jenerali Mabele alitolea mfano ufugaji samaki wa kisasa kwa njia ya matanki unaofugwa kwenye Kikosi cha Chita JKT ambayo yameungunishwa na maji kutoka Milima ya Udzungwa na baadaye yanatoka na kwenda kwenye mashamba ya mpunga.
Social Plugin