Muonekano wa milango ya kituo cha afya Bulige Halmashauri ya Msalala Mkoani Shinyanga baada ya kung'olewa na mafundi ambao wanadai haki zao kwa muda mrefu
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Msalala Khamis Katimba akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake leo Jumatatu 12 ,Agosti 2024 Juu ya kituo cha afya Bulige kilicho ng'olewa milango.
NA MWANDISHI WETU, KAHAMA
Mkurugenzi wa Kampuni ya AJ MABAO INVESTMENT, Abel Mabao, amejikuta akilazimika kutoa milango ya kituo cha afya cha Bulige halmashauri ya Msalala Mkoani Shinyanga kwa madai ya kutokulipwa fedha zake za ujenzi na ukamilishaji wa kituo hicho.
Tukio hilo la kushangaza limetokea mwishoni mwa wiki iliyopita, na Mabao ameeleza kuwa anadai jumla ya shilingi milioni 67 tangu mwezi Agosti ,2023, bila kulipwa hadi sasa.
Mabao ameeleza kuwa kila alipojaribu kuzungumza na mkurugenzi wa halmashauri ya Msalala, amekuwa akipewa ahadi zisizotekelezwa na hivyo, mafundi wamelazimika kuchukua milango yao kwa sababu mabao hana fedha za kuwalipa.
Mabao ameeleza kuwa amekuwa mzabuni mkubwa katika halmashauri ya Msalala, akidai zaidi ya milioni 130)kwa hospitali ya Msalala na kituo cha afya Ntobo, hivyo jumla ya deni la halmashauri hiyo kwake ni zaidi ya milioni 200.
Fundi wa kutengeneza milango, Joseph Masele Shija, amesema alitengeneza milango 40 ya chuo cha uuguzi Ntobo tangu mwaka 2021 na anadai shilingi milioni 8 kutoka kwa Mabao.
Shija alikopeshwa fedha ili kutengeneza milango ya haraka kwa ajili ya kituo cha afya Bulige, tangu mwezi wa nane mwaka 2023 milango hiyo haijalipwa hadi sasa.
Fundi mwingine, Mabula Hamisi, ambaye alitengeneza madirisha ya vioo, amesema alipigiwa simu na fundi wa milango kuhusu kazi hiyo na alikopa vifaa dukani kutekeleza kazi hiyo, lakini pia hajapokea malipo.
Mkurugenzi wa halmashauri ya Msalala, Hamisi Katimba, amekiri kuwa halmashauri inadaiwa na Mabao na kwamba walizungumza kuhusu malipo siku mbili kabla ya tukio.
Katimba ameahidi kulipa ndani ya wiki hii lakini ameshangaa taarifa za kung'olewa kwa milango katika kituo hicho.
Amesema kuwa hatua hiyo si sahihi za mafundi kung'oa milango na kwamba hatua zitachukuliwa ili kulipa madeni haya kwa haraka.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Msalala Khamis Katimba akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake leo Jumatatu 12 ,agosti 2024 juu ya kituo cha afya Bulige kilichong'olewa milango
Fundi wa kutengeneza madirisha ya vioo akizungumzia suala la kutokulipwa kwa wakati fedha zao walizotengeneza madirisha ya kituo cha afya Bulige
Fundi wa kutengeneza milango akizungumzia suala la kutokulipwa kwa wakati fedha zao walizotengeneza milango ya kituo cha afya Bulige
Mkurugenzi wa AJ MABAO INVESTMENT akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake kuhusu kung'olewa kwa milango ya kituo cha afya Bulige
Mkurugenzi wa AJ MABAO INVESTMENT akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake juu ya kung'olewa kwa milango ya kituo cha afya Bulige
Muonekano wa milango ya kituo cha afya bulige baada ya kung'olewa na mafundi ambao wanadai haki zao kwa muda mrefu
Muonekano wa milango ya kituo cha afya Bulige baada ya kung'olewa na mafundi ambao wanadai haki zao kwa muda mrefu
Muonekano wa milango ya kituo cha afya bulige baada ya kung'olewa na mafundi ambao wanadai haki zao kwa muda mrefu
Muonekano wa jengo la kituo cha afya Bulige ambacho kimeng'olewa milango na mafundi kwa madai ya kutokulipwa fedha zao tangu Agosti ,2023
Social Plugin