Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

KARIAKOO WABORESHEWA HUDUMA ZA USAFI WA MAZINGIRA

 


Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA) imeendesha zoezi la usafishaji wa miundombinu ya majitaka katika eneo la Kariakoo Wilaya ya Ilala kwa lengo la kuboresha usafi wa mazingira katika eneo hilo.

Akizungumza kazi hiyo Meneja wa huduma za Usafi wa Mazingira Mhandisi Jolyce Mwanjee ameeleza kuwa lengo ni kutatua changamoto sugu ya uzibaji wa chemba hali inayosababisha uchafuzi wa mazingira na kuhatarisha afya za watumiaji wa soko hilo.

"Eneo hili linatumiwa na wafanyabiashara na wateja wengi huudhuria kila siku, hatuwezi ruhusu utiririshaji majitaka ambayo huathiri ufanyaji biashara pamoja na watumiaji wa soko hili, hali hii tutaimaliza kabisa" ameeleza Mhandisi Mwanjee

Denis Henry, mmoja wa wafanyabiashara katika soko la Kariakoo ameipongeza DAWASA kwa jitihada za haraka kufika na kutatua changamoto ya majitaka muda mfupi baada ya kupewa taarifa hizo.

"Tulishindwa kufanya biashara kwa uhuru kwani mazingira yalikua machafu kufuatia utiririkaji wa majitaka, tumewapatia DAWASA taarifa na hawajachukua muda mrefu kufika na kutatua kero hii, lakini tumefurahi kuskia wanaendelea na zoezi hili sehemu mbalimbali" ameeleza ndugu Denis.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com