Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

LGTI YAJA NA MBINU MPYA KURAHISISHA UPATIKANAJI WA ELIMU


Na Dotto Kwilasa, Dodoma

Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo(LGTI) kipo mbioni kuanzisha mfumo wa mafunzo kwa njia ya mtandao kama njia ya kuboresha upatikanaji wa elimu na kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma.
Aidha Mfumo huo utawasaidia wanafunzi kupata ujuzi na maarifa muhimu bila kuhitaji kuhudhuria mafunzo kwa njia ya moja kwa moja.

Hayo yamesemwa leo Agosti 7,2024 Jijini hapa na Naibu Mkuu wa Chuo Taaluma,tafiti na Ushauri wa Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo Professa Magreth Bushesha wakati akizungumza na waandishi wa habari mara alipotembelea Banda la chuo hicho katika maonesho ya kitaifa ya wakulima-Nanenane Nzuguni Dodoma.

Prof. Bushesha amesema kwa mwaka wa masomo 2025/26 chuo hicho na Kampasi zake zote kitaanza kutoa mafunzo kwa njia ya mtandao kwa program za cheti mpaka Degree na kueleza kuwa kwa sasa wanatoa mafunzo hayo yanatolewa mtandaoni kwa kozi za muda mfupi .
Amefafanua kuwa LGTI imejipambanua kujiendesha kidigili ambapo katika kozi fupi wanazo zitoa zimechangia kwa kiasi kikubwa kuboresha utendaji kazi kwenye sekta ya serikali za mitaa .

" Tumefarijika kuona watendaji wetu sasa waanavyoziangalia changamoto na kuzifanya kuwa fursa ,kupitia masomo yanayotolewa Chuoni kwetu changamoto mbalimbali zinatatuliwa kwa weledi ,kabla serikali haijatia mkono wake ,ni jambo la kujivunia,"amesema Prof Bushesha .

Ameeleza kuwa chuo hicho kina matawi matatu ambapo ikiwemo Hombolo, Dodoma mjini na Shinyanga huku wakiwa na mpango wa kwenda sehemu nyingine kuweza kuwafikia wananchi wengi zaidi.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com