BENKI YA CRDB YAKABIDHI MADAWATI SHULE YA SEKONDARI MAGANZO

Benki ya CRDB tawi la Maganzo imekabidhi madawati kwenye shule ya sekondari Maganzo yenye thamani ya Shilingi Milioni 3.

 

Hafla hiyo ya makabidhiano imefanyika leo Agosti 30, 2024 katika shule ya sekondari Maganzo wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga ambapo CRDB benki imekabidhi viti pamoja na meza 44 ikiwa ni asilimia 1 inayorudishwa kwenye jamii. 

 

Akisoma taarifa ya shule hiyo Kaimu mkuu wa shule ya sekondari Maganzo Evalist Luhende amesema kumekuwa na changamoto ya meza na viti kwa wanafunzi wawapo shuleni kutokana na idadi kubwa ya wananfunzi waliopo shuleni hapo. 

 

"Shule yetubina jumla ya wananfunzi 1237 wavulana 611 na wasichana 626 kabla ya kupokea msaada huu kutoka benki ya CRDB uhitaji wa meza na viti ni 1237 huku yaliyopo ni 834 hivyo uhitaji ni 403, tunawashukuru sana wadau wetu wa elimu benki ya CRDB tawi la Maganzo kwa kutupatia msaada huu, na kufanya kufikia idadi ya madawati 878 hivyo uhitaji bado ni mkubwa kulingana na wanafunzi waliopo, tunawaahidi kuendelea kufanya vizuri na kutunza madawati haya ili yaweze kutumika kwa vizazi na vizazi vijavyo", amesema Mwl. Luhende. 

 

Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Mkuu wa Kitengo cha Malipo na Udhibiti wa Benki ya CRDB, Madaha Mayega Chabba, ameeleza kuwa msaada huo ni sehemu ya juhudi za benki hiyo kusaidia kuboresha mazingira ya kujifunzia kwa wanafunzi nchini. 

 

Amebainisha kuwa takwimu za Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022 zinaonyesha kuwa asilimia 49.1 ya Watanzania ni watoto wenye umri chini ya miaka 18, na wengi wao wanahitaji huduma bora za elimu ili kufikia malengo yao ya maisha. 

 

“Benki ya CRDB inatambua umuhimu wa elimu katika maendeleo ya jamii kwa miaka mingi, tumekuwa tukisaidia miradi mbalimbali ya kijamii, hususan katika sekta ya elimu, mazingira, na afya kila mwaka, tunatenga asilimia moja ya faida yetu baada ya kodi kwa ajili ya kusaidia miradi ya kijamii, na leo tunakabidhi madawati haya 44 ili kuwasaidia wanafunzi wa Sekondari ya Maganzo kupata mazingira bora ya kusomea,” amesema Chabba. 

 

Meneja wa Benki ya CRDB kanda ya Magharibi Jumanne Wagana akizungumza wakati wa hafla hiyo fupi ya makabidhiano ya madawati shuleni hapo amesema benki ya CRDB imeendelea kuiunga mkono serikali kwenye sekta mbalimbali ikiwemo sekta ya elimu kwa kuchangia vifaa mbalimbali vya kujifunzia ujenzi wa madarasa ili kuwawezesha wanafunzi kuendelea kufanya vizuri kwenye masomo yao na kufikia malengo. 

 

"Sisi Benki ya CRDB tumeweka utaratibu wa asilimia 1 ya faida tunayoipata tunairudisha kwa jamii ambapo hivi karibuni tulikabidhi madarasa mawili pamoja na madawati katika shule ya msingi Kiloleli, jambo hili ni muendelezo kama tulivyosikia kwenye taarifa iliosomwa hapa kuwa zipo changamoto zinazoikabili shule ya sekondari Maganzo ni waahidi kuwa tutaendelea kufanya hivyo pindi bajeti itakapo ruhusu lengo likiwa ni kuongeza ufaulu na kuboresha mazingira ya kujifunzia kwa watoto mashuleni", amesema Jumanne Wagana. 

 

Kwa upande wake mgeni rasmi kwenye hafla hiyo Katibu tawala wilaya ya Kishapu Bi. Fatma Mohamed aliyemuwakilisha mkuu wa wilaya ya Kishapu Joseph Mkude amewataka wanafunzi kutunza madawati hayo huku akiipongeza CRDB kwa kuiunga mkono serikali na kuwasihi wadau wengine kuiga mfano huo. 

 

"Niwapongeza sana benki ya CRDB kwa kutoa msaada huu wa madawati ambayo yatakwenda kuwasaidia watoto wetu kuweza kujifunzia, mmekuwa mkifanya hivyo sehemu mbalimbali kupitia faida mnayopata tunawashukuru sana, na nitoe wito kwa taasisi zingine kuiga mfano huu kwani jukumu la kuhakikisha watoto wetu wanapata elimu bora ni la kila mmoja wetu, lakini pia niwasihi wanafunzi na waalimu wa shule ya sekondari Maganzo kutunza madawati haya ili yaweze kudumu kwa muda mrefu", amesema Bi Fatma.

 

 Kaimu mkuu wa shule ya sekondari Maganzo Evalist Luhende akisoma taarifa wakati wa hafla hiyo ya makabidhiano.

Diwani kata ya Maganzo Mhe. Lwinzi Kidiga akizungumza wakati wa hafla hiyo.

   Afisa tarafa ya Mondo Bi. Atka Haji akizungumza wakati wa hafla hiyo ya makabidhiano.

  Meneja wa Benki ya CRDB kanda ya Magharibi Jumanne Wagana akizungumza wakati wa hafla hiyo.

Mkuu wa Kitengo cha Malipo na Udhibiti wa Benki ya CRDB, Madaha Mayega Chabba akizungumza wakati wa hafla hiyo.

Mkuu wa Kitengo cha Malipo na Udhibiti wa Benki ya CRDB, Madaha Mayega Chabba akizungumza wakati wa hafla hiyo.

Katibu tawala wilaya ya Kishapu Bi. Fatma Mohamed akizungumza wakati wa hafla hiyo ya makabidhiano.

Katibu tawala wilaya ya Kishapu Bi. Fatma Mohamed akizungumza wakati wa hafla hiyo ya makabidhiano.








Zoezi la makabidhiano ya viti na meza likiendelea.

Zoezi la makabidhiano ya viti na meza likiendelea.

Baadhi ya meza na madawati yaliyotolewa na benki ya CRDB katika shule ya sekondari Maganzo.

Meneja wa CRDB tawi la Maganzo Bi. Constansia Albinus akizungumza kwenye hafla ya kukabidhi madawati.



Baadhi ya meza na madawati yaliyotolewa na benki ya CRDB katika shule ya sekondari Maganzo.





Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post