MADIWANI WAITAKA MANISPAA YA MOROGORO KUNUNUA GREDA KUCHONGA BARABARA KUWANUSURU KWENYE UCHAGUZI


Baadhi ya madiwa wa halmashauri ha manispaa ya Morogoro
Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro Mhandisi Paschal Kihanga
Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro Mhandisi Paschal Kihanga

Na Christina Cosmas, Morogoro

MADIWANI wa Halmashari ya Manispaa ya Morogoro wameitaka Halmashauri hiyo kuhakikisha inanunua Greda la kuchonga barabara kabla ya Agosti 30 mwaka huu ili kutowakwamisha kwenye uchaguzi hapo mwakani.

Madiwani hao akiwemo Samuel Msuya wa kata ya Mbuyuni wamesema hayo kwenye kikao robo ya mwisho ya baraza madiwani kinachofanyika kwenye ukumbi wa manispaa hiyo.

Msuya anasema changamoto ya barabara iliyopo kwa sasa kwenye karibu kata zote za Manispaa ni kubwa sababu barabara karibu zote hazipitiki na wanashindwa ya kuwaleza wananchi wao ambapo waliazimia kununua Greda ili kusaidiana na wakala wa barabara nchini (TARURA) kutatua changamoto hiyo.

Anasema waliazimia ifikapo Agosti 30 greda hilo liwe tayari kwa uzinduzi baada ya kukamilika manunuzi yake.

Naye Diwani wa kata ya Lukobe Selestin Mbilinyi anasema katika kikao cha awali walikubaliambiwa zimebaki shilingi Milioni 550 kati ya milioni 700 walizochanga ambapo waliomba kuongezwe fedha za bakaa ili kuweza kununua Greda hilo.

Naye Mstahiki Meya wa Manispaa ya Morogoro Mhandisi Pascal Kihanga anasema upembuzi kamili wa ununuzi wa greda kutoka kwa mhandisi wa Manispaa ulibaini kuwa manunuzi ya greda lenye thamani ya shilingi Milioni 700 hayatakidhi mahitaji kutokana na greda hilo kuwa katika mfumo usiokubalika.

Meya huyo anasema Greda hilo litanunuliwa kwa muda muafaka uliokubaliwa kwa kiasi cha shilingi Bilioni 1.2 badala ya shilingi Milioni 700 iliyotengwa.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post