Na Mwandishi Wetu ,Manyara
Kampuni ya Mati Super Brands Limited inayozalisha vinywaji changamshi yenye makao yake Makuu Mjini Babati Mkoani Manyara imepewa tuzo ya maalumu kutoka Chuo cha Ukamanda na Unadhimu (CSC) kwa kutambua mchango wa kampuni hiyo katika kusaidia jamii inayowazunguka Pamoja na kushirikiana na taasisi mbalimbali za kiserikali.
Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa tuzo hiyo na Mwakilishi wa Mkuu wa Chuo cha Ukamanda na Unadhimu (CSC) chenye makao yake Mkoani Arusha , Colonel Verus Chrysostom Mbuzi katika ziara maalumu ya kimafunzo iyofanywa na Maafisa hao wa ngazi za juu wa Kijeshi kutoka mataifa mbali mbali katika kampuni ya Mati Super Brands Ltd.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mati Super Brands Limited David Mulokozi ametoa shukrani zake kwa Chuo hicho cha kijeshi kwa kutambua mchango wa kampuni hiyo katika masuala mbali mbali ikiwemo kurudisha sehemu ya faida wanayoipata kwa jamii inayowazunguka.
Mulokozi amesema kuwa Tuzo hiyo inawapa chachu ya kuendelea kufanya vizuri kuendelea kushirikiana na taasisi za umma Pamoja na kuzalisha bidhaa bora zinazozingatia ubora na usalama wa mtumiaji.
Mwakilishi wa Mkuu wa Chuo cha Ukamanda na Unadhimu (CSC) , Colonel Verus Chrysostom Mbuzi amepongeza Kiwanda kwa kuwa karibu na jamii na taasisi za serikali pamoja na kutoa fursa wa mafunzo kwa vitendo vya Maafisa wa Kijeshi juu ya masuala mbali mbali ikiwemo usalama wa chakula .
Social Plugin