Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MELI KUTOKA CHINA ZITAENDELEA KUTIA NANGA BANDARI YA TANGA

Na Hamida Kamchalla, TANGA.

Kampuni ya Uwakala wa Meli Seafront  Shipping Service (SSS), kwa mara ya kwanza imefanikiwa kuleta meli yenye shehena ya mizigo mchanganyiko 
inayokadiriwa kuwa takribani tani (14,000) kutoka nchini Chiina wamoja hadi bandari yaTanga.

Hii inaweka alama ya kipekee kuwahi kutokea kwa meli ya mizigo mchanganyiko kuweza kushusha kiwango kikubwa cha mizigo mchanganyiko,zaidi ya magari 500 na aina nyingine ya mizigo mchanganyiko kuweza kushushwa katika bandari hiyo.

Meneja mkuu wa kampuni hiyo Neelakandan CJ amesema baadhi ya mizigo itaelekea katikanchi Jirani kama Zambia, Zimbabwe, Jamhuri ya watu wa Kongo (D.R.C), Malawi, Rwanda nakadhalika na mizigo mingine itabaki hapa nchini kwa maana ya (localgoods),

"Kimsingi haya ni mafanikio makubwa na muhimu kwa maendeleo ya Bandari ya 
Tanga, bandari hii inatarajia pia kupokea aina nyingi ya mizigo kuelekea nchi za jirani, na hii itafanya wafanyabiashara, watoa huduma za usafiri, mawakala wa 
forodha,jamii za wafanyabiashara wa ndani" amesema.

"Kwa pamoja tunanufaika kwa kiwango cha juu kutokana na meli zitakazokuwa zinatia nanga bandari ya Tanga moja kwa moja kutoka bandari za Kimataifa
zaidi, kutakuwa nameli za mizigo 
mchanganyiko kuanzaia 3 mpaka 4 kipindi cha hivi karibuni, ambazo tayari zimepangwa kuingia bandari ya Tanga" ameeleza.

Kwa upande wake Meneja wa Bandari Mkoa wa Tanga Masoud Mrisha amesema ujio wa meli hiyo ni matokeo makubwa ya maboresho ya Bandari hiyo na Kwa mara ya kwanza meli kubwa imetia nanga.

Mrisha amesema mbali na meli hiyo, kampuni hiyo itaendelea kuleta meli nyingine ndanya mwezi Agosti lakini pia itaendelea kuwa mteja wa kupitisha mizigo yake katika bandari ya Tanga.

Amebainisha kwamba kupitia maboresho hayo wamefanikiwa kuingiza meli kubwa zipatazo 35 zilizobeba tani 330,173 ndani ya mwezi wa saba mwaka huu, na kwa mwaka wa fedha 2024/25 tayari wamekwisha pokea meli 31 wakati lengo ni kuingiza meli 19 hali iliyopelekea kuvuka malengo 

"Tumeanza mwanzo mzuri, mwaka jana mwezi kama huu wa saba tulihudumia meli zenye tani 46 na mwaka huu kabla mwezi haujaisha tumesha hudumia meli zenye tani 96, kwahiyo dalili njema, na mwaka huu tumewekewa lengo la tani milioni 1.4" amefafanua Mrisha.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com