Na Dotto Kwilasa, Dodoma
Serikali imesema katika kipindi cha Mwaka 2019 hadi 2023 jumla ya shilingi 924,685,884 zilikusanywa kutokana na madini yaliyozalishwa katika Wilaya ya Kakonko, mkoani Kigoma.
Naibu Waziri wa Madini Dkt. Steven Kiruswa ameeleza hayo leo Agosti 30, 2024 Bungeni Dodoma alipokuwa akijibu swali lililoulizwa na Aloyce John Mbunge wa Buyungu.
Mheshimiwa Buyungu alitaka kujua kiasi cha fedha zilizopatikana kutokana na madini katika Wilaya ya Kakonko kuanzia Mwaka 2019 hadi 2023.
Akijibu swali , Dkt. Kiruswa amesema kuwa , Wilaya ya Kakonko ni miongoni mwa Wilaya zilizojaliwa kuwa na madini ya dhahabu nchini.
"Kutokana na madini yanayozalishwa Kakonko Shilingi 725,171,133.52 zilitokana na mrabaha na Shilingi 199,514,750.46 zilitokana na ada ya ukaguzi wa madini yaliyozalishwa kwa kipindi kinachorejewa" amesema Dkt. Kiruswa.
Aidha, Dkt. Kiruswa ameongeza kuwa, Madini mengine yanayopatikana katika Wilaya hiyo ni madini ujenzi aina ya mchanga , chuma, Shaba, makaa ya mawe na chokaa ambayo kwa sehemu yamechangia katika ujenzi wa barabara zinazounganisha Wilaya hiyo na maeneo mengine nchini.
Mkoa wa Kigoma umeunganishwa na wilaya nane , kakonko, kasulu, kibondo , uvinza, Buhigwe, Kusulu vijijini , Kigoma mjini na kigoma vijijini.
Social Plugin