Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MWENYEKITI WA MARA PRESS CLUB, MENEJA WA TCRA KANDA YA ZIWA WAFANYA MAZUNGUMZO MWANZA

Meneja wa TCRA Kanda ya Ziwa, Imelda Salum (kushoto) akimpatia Mwenyekiti wa MRPC, Mugini Jacob zawadi ya kalenda.
Meneja wa TCRA Kanda ya Ziwa, Imelda Salum (kushoto) na Mwenyekiti wa Kilabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Mara, Mugini Jacob wakiwa katika mazungumzo maalum katika ofisi za TCRA jijini Mwanza juzi.


Na Mwandishi Wetu, Mwanza

Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Mara (MRPC), Mugini Jacob amefanya mazungumzo maalum na Meneja wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Ziwa, Mhandisi Imelda Salum.

Mazungumzo ya viongozi hao yalifanyika katika ofisi za TCRA Kanda ya Ziwa zilizopo jijini Mwanza juzi, yakilenga kuboresha utendaji kazi wa vyombo vya habari vya mtandaoni vilivyopo mkoani Mara.
Mwenyekiti wa MRPC, Mugini Jacob akisaini katika kitabu cha wageni baada ya kukaribishwa na Meneja wa TCRA Kanda ya Ziwa.

“Nimefurahi kukutana na Meneja wa TCRA katika kanda yetu ya Ziwa, na mazunguzo yetu yametupatia mwanzo mzuri zaidi kuhusu namna tunavyoweza kusaidia kutatua changamoto zilizopo kwa waandishi wa habari wanaotumia mitandao ya kijamii kama vile 'Online TV na blogs,” Jacob aliiambia Mara Online News jijini hapa muda mfupi baada ya mazungumzo hayo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com