Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MZUMBE KUENDELEA NA MAONESHO NANENANE – DODOMA


Chuo Kikuu Mzumbe kinaendelea kuwakaribisha wananchi wa Mikoa ya Kanda ya Kati kutembelea Banda la Chuo hicho katika maonesho ya Kilimo ya Kimataifa (Nanenane) 2024 yanayoendekea katika viwanja vya Nanenane, Nzuguni jijini Dodoma.

Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Masoko Chuo Kikuu Mzumbe, Bi. Lulu Mussa amesema licha ya maonesho hayo kufikia kilele chake Agosti 8, 2024 Chuo hicho kinaendelea kutoa huduma katika maonesho hayo mpaka Agosti 10,2024 yatakapo itimishwa rasmi ikiwa ni kutii maelekezo ya Serikali ya kuendelea kwa siku mbili zaidi.

"Sisi Chuo tunaendelea kuwahudimia wananchi watakaofika kwenye Banda letu hivyo wasisite kutembelea kwani maonesho bado yanaendelea”. Alisisitiza Bi. Mussa.

Amezitaja miongoni wa huduma zinazotolewa katika Banda hilo ni Udahili papo kwa hapo kwa wanafunzi wanaotarajia kujiunga na chuo kwa mwaka wa masomo 2024/2025 kuanzia Astashahada mpaka Shahada za Uzamivu, huduma wa msaada wa kisheria unatolewa bure pamoja na kushuhudia bunifu mbalimbali za kiteknolojia zilizobuniwa na Wanafunzi wa wa Chuo hicho.

Tupo tayari kukuhudumia, Karibu Chuo Kikuu Mzumbe, Tujifunze kwa Maendeleo ya Watu.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com