Na Dotto Kwilasa,Dodoma
NAIBU Waziri,Ofisi ya Waziri Mkuu(Sera,Bunge na uratibu)Ummy Nderiananga amesema Serikali inaendelea kuimarisha miundombinu ya kilimo kama vile teknolojia za kisasa, barabara, mabwawa ya umwagiliaji, na maghala ya kuhifadhia mazao ili kuwasaidia wakulima kulima kwa tija.
Akizungumza mara baada ya kukagua maonesho ya wakulima yanayoendelea kwenye viwanja vya Nanenane Nzuguni Agosti 4,2024 Jijini Dodoma amesema Serikali kwa kushirikiana na wadau wa kilimo wataanza kuhamasisha mafunzo na vifaa vya kisasa kwa wakulima, ikiwa ni pamoja na mbegu bora na mbolea ya kisasa ili kuongeza uzalishaji.
"Serikali inahamasisha taasisi za Mikopo na Fedha kuwakopesha wakulima mikopo yenye riba nafuu kwa ili kuwawezesha kupata mitaji ya kuendesha shughuli zao za kilimo na uboreshaji wa Soko la Mazao, " Amesema
Waziri Nderiananga pia amesema,"Tunafanya jitihada za kuimarisha soko la mazao kwa kuanzisha vituo vya biashara na kuboresha miundombinu ya usafirishaji,Wakulima na Wadau,Tunatoa wito kwa kila mmoja wenu kuendelea kushirikiana na Serikali katika kuleta mabadiliko chanya katika sekta ya kilimo, "amesisistiza
Ameongeza kuwa kwa kushirikiana hali ya maisha ya wakulima itaimarika na kuleta maendeleo kwa taifa huku akitoa wito kwa Watanzania kutembelea maonyesho wakulima nane nane ambayo kitaifa yanafanyika jijini Dodoma,ili wajifunze na kuna teknolojia mpya Pamoja na ubunifu.
Amesema maelekezo ambayo yametolewa na waziri Wa kilimo Husen Bashe kuwà eneo hilo litakuwa endelevu hali itakayo saidia kuunganisha nguvu na kufanya maonyesho yenye tija.
Social Plugin