Na mwandishi wetu, Zanzibar
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, amekabidhi cheti cha pongezi kwa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania - TAWA kutokana na ushiriki wake wa kipekee katika Tamasha la Tisa la Kizimkazi lililofanyika Kusini Unguja, Zanzibar kuazia tarehe 18-25 Agosti, 2024.
Cheti hicho cha pongezi kilipokelewa na Afisa Utalii Mustapha Buyogera katika hafla ya chakula cha usiku iliyofanyika Ikulu ndogo, Kizimkazi, Zanzibar.
Katika tamasha hilo, Banda la Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia TAWA limekuwa kivutio kikubwa kwa wananchi wengi na wadau mbalimbali wa utalii ambapo wageni walipata fursa ya kushuhudia wanyamapori hai waliopo katika bustani ya wanyamapori hai.
Social Plugin