RAIS SAMIA AWAKOSHA WAANDISHI WA HABARI






Na Dotto Kwilasa,Dodoma

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan amewakosha waandishi wa habari wa Mkoa wa Dodoma kwa hatua ya kupiga picha nao mmoja baada ya mwingine .

Tukio hilo limetokea leo Agosti 10,2024 nyumbani kwake Ikulu-Chamwino kabla ya kuanza kikao chake na Maafisa Ugani pamoja na wanaushirika ambapo alipata fursa ya kupita meza moja baada ya nyingine na kupiga picha.

Rais Samia ametumia nafasi hiyo kuwapongeza wanahabari kwa mchango wao kwenye jamii na kuwataka waendelee kufanya kazi kwa bidii.

"Nimefurahi kukutana nanyi, naomba niwashukuru kwa kujitoa kwa ajili ya nchi yenu, niwaombe muendelee kuhabarisha Umma kwa kwa usahihi, endeleeni kufanya kazi kwa bidii, " amesema Rais Samia.

Hii ni ishara ya kuthamini kazi yao na umuhimu wa kazi ya Uandishi wa habari katika kuhabarisha Umma na kutoa taarifa sahihi.

Rais pia ameonesha umuhimu wa waandishi wa habari katika kuimarisha uwazi na kuendeleza demokrasia.

Pamoja na mambo mengine shukrani hizi zinatazamwa kama ni somo kwa viongozi wengine na kuwa sehemu ya kukuza uhusiano mzuri kati ya viongozi na vyombo vya habari.

Tukio hilo limechukuliwa na waandishi hao wa habari kama upendo wa kipekee kutokana na sababu kwamba viongozi wa kitaifa wanapokuwa na shughuli au matukio maalum ni nadra sana kwa kiongozi wa juu kutembelea kila meza na kupiga picha.

Kulingana na itifaki jambo hili huwa halifanywi na viongozi wengi na hivyo tukio hili linaweza kuendelea kuwa kielelezo cha uzalendo nankuchukuliwa kuwa ni mfano wa jinsi viongozi wanavyoweza kujenga uhusiano mzuri na Jamii inayowazunguka.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post