LIGI YA DKT. SAMIA - KATAMBI CUP IMEENDELEA KUTIMUA VUMBI HATUA YA 16 BORA, OLD SHINYANGA NA LUBAGA FC ZAAGA MASHINDANO

Michuano ya Dkt. Samia, Katambi Cup imeendelea kutimua vumbi kwenye viwanja mbalimbali ndani ya manispaa ya Shinyanga katika hatua ya 16 bora kuelekea kumtafuta mshindi atakayejinyakulia Shilingi Milioni 6.

Mashindano hayo yameendelea siku ya leo Agosti 07, 2024 ambapo timu ya Mwamalili FC imeichakaza timu ya Lubaga FC kwa mikwaju ya penati 4 kwa 3 mchezo uliokuwa ukipigwa katika uwanja wa Ufaransa kwa matokeo hayo timu ya Mwamalili FC imefanikiwa kusalia kwenye mashindano hayo.

Kwingineko ni timu ya Old Shinyanga imetolewa kwenye mashindano kwa kukubali kichapo cha goli 3 - 2 kutoka kwa timu ya Masekelo mchezo uliokuwa kupigwa katika uwanja wa Jasko uliopo kata ya Ngokolo.

Mashindano hayo yanatarajia kuendelea hapo kesho yakizikutanisha timu nne ambazo ni Kashwasa FC dhidi ya Bodaboda FC na Chamagua dhidi ya Ndala FC kuanzia muda wa saa 9 alasiri.

Mashabiki wa timu ya Mwamalili wakishangilia baada ya kuibuka washindi kwenye mchezo huo.

Mchezo kati ya Old Shinyanga dhidi ya Masekelo ukiendelea.

Mchezo ukiendelea kati ya timu ya Mwamalili FC dhidi Lubaga FC.

Mikwaju ya penati ikichezwa kati ya timu ya Mwamalili FC dhidi ya Lubaga katika uwanja wa Ufaransa kata ya Ndembezi.

Baadhi ya mashabiki waliojitokeza kutazama mchezo kati ya Mwamalili dhidi ya Lubaga.

Baadhi ya mashabiki waliojitokeza kutazama mchezo kati ya Mwamalili dhidi ya Lubaga.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post