Na Dotto Kwilasa,Dodoma
Maonesho ya wakulima yakiwa yanaendelea Jijini hapa kwenye viwanja vya maonesho Nanenane-Nzuguni,Serikali imeendelea kusisitiza umuhimu wa matumizi ya nishati safi ya kupikia kama nyenzo muhimu ya kukabiliana na athari za kimazingira, kiafya, kijamii na kiuchumi.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati nchini Felchesmi Mramba amezungumza hayo leo Agosti 6,2024 mara baada ya kutembelea mabanda kwenye maonesho hayo ambapo ameeleza kuwa jitihada hizo zitaifikisha salama Tanzania kwenye matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia.
"Maonesho haya yamekuwa ni sehemu ya wananchi kujionea utekelezaji wa miradi mbalimbali katika Sekta ya Nishati ikiwemo miradi ya Gesi Asilia na Mafuta, Sekta ya Nishati inafungamanisha Sekta nyinginezo ikiwemo Madini, Maji, Kilimo na Mifugo ambapo katika Mifugo vinyesi vya wanyama hutumika kuzalisha nishati kwa ajili ya matumizi mbalimbali, "amefafanua Mramba
Kwa upande wake, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Dkt. James Mataragio ameipongeza Wizara ya Nishati na Taasisi zake kwa kuendelea kutoa elimu ya kwa wananchi kuhusu mafanikio ya Sekta ya Nishati pamoja na Nishati Safi ya Kupikia.
Social Plugin