SHIRIKA la Viwango Tanzania (TBS) kanda ya Mashariki, limewataka wajasiriamali, wafanyabiasha,wazalishaji na watumiaji wa bidhaa mbalimbali kuzingatia alama ya ubora inayotolewa na shirika hilo ili kuhakikisha watumiaji wantumia bidhaa salama na zenye ubora.
Hayo yameelezwa na kaimu meneja wa shirika hilo kanda ya mashariki Franses mapunda kwenye maonyesho ya wakulima ya nane nane kanda ya mashariki yanayofanyika katika viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere mkoani Morgoro ambapo amewataka wazalishaji,wauzaji,wasambazaji pamoja na watumiaji wa bidhaa hizo kufika kwenye banda la TBS lililopo kwenye Maonesho hayo ili waweze kupatiwa elimu ya namna bora ya kusajili bidhaa zao, majengo pamoja na vipodozi.
Aidha amesema kuwa kupitia Maonesho hayo ni rahisi kuwafikia wadau wa TBS wakiwemo wajasiriamali mbalimbali wanaotembelea maonesho hayo kuwapatia elimu juu ya masuala yote yanayohusu viwango kabla ya kuzalisha,kusambaza, kuuza na kutumia bidhaa zao.
kwa upande wao baadhi ya wananchi waliofika katika banda la TBS wamesema kuwa wamepatiwa elimu nzuri juu ya masuala mbalimbali ya viwango jambo litakalo wasaidia katika kuendesha shughuli zao za ujasiriamali kuinua kipato chao na taifa kwa ujumla.
Social Plugin