Na Angela Msimbira UGANDA
Timu ya Netiboli ya Tanzania katika michuano ya Shule za Msingi na Sekondari ya Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (FEASSSA) imeibuka na ushindi kwa kuichapa timu ya Rwanda mabao 66- 32.
Katika mashindano hayo ya 22 yanayofanyika Mji wa Mbale nchini Uganda, mchezo huo umechezwa viwanja vya shule ya msingi Mukedea.
Kwa upande wa mpira wa Kikapu 5x5 Timu ya wavulana ya Tanzania imeichapa Uganda kwa mabao 77- 70, huku 3x3 ikipata mabao 13-10.
Timu ya Tanzania ya Mpira wa Mikono kwa wavulana imeonyesha uwezo wake baada ya kucheza na Kenya na kupata magoli 22-23.
Social Plugin