Na Mwandishi Maalum, Dodoma
Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi (PDPC) imepongezwa kwa kufanya kazi kwa weledi na Ushirikiano wenye lengo la kuleta matokeo chanya kwenye sekta ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi nchini.
Pongezi hizo zimetolewa tarehe 14 Agosti, 2024 na Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi (Mb), wakati wa ziara yake ya kikazi katika ofisi za Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi (PDPC) zilizopo Jijini Dodoma.
"Tume hii ni moja ya vipaumbele vya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan hivyo tunapaswa kumsaidia kutimiza maono yake" Amesema Mhe. Mahundi.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi (PDPC) Bw. Emmanuel Mkilia ameweka bayana baadhi ya majukumu ya Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi kuwa ni pamoja na Kusimamia utekelezaji wa Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi, kusajili Taasisi zote zinazokusanya na kuchakata Taarifa.
Majukumu mengine ya Tume hiyo ni Kufanya Tafiti na kufuatilia Maendeleo ya Teknolojia yanayoathiri Usalama wa Taarifa Binafsi, Kupokea, kuchunguza na kushughulikia Malalamiko yanayohusiana na ukiukwaji wa haki za Faragha.
Social Plugin