Na Dotto Kwilasa, Dodoma
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan amezindua rasmi mradi wa Reli ya Mwendokasi (SGR) katika hafla iliyofanyika Mkonze Jijini hapa huku akiridhia ombi la Kituo cha Stesheni ya Reli hiyo kwa upande wa Dodoma kuitwa jina lake.
Akizungumza leo Aprili 1,2024 Jijini hapa amesema Mradi huo ambao umewekezwa kwa gharama kubwa na umejengwa kwa viwango vya juu,utaleta matumaini mapya katika sekta ya usafiri nchini.
Ametaja kwa mtiririko majina ya stesheni za reli hiyo kwa kueleza kuwa kituo cha Dar es Salaam kitaitwa jina la Magufuli,Kituo cha Morogoro kitaitwa Kikwete,Kituo cha Dodoma kitaitwa Samia wakati kituo cha Tabora kitaitwa Mwinyi ,kituo cha Shinyanga kitaitwa Abeid Karume,Mwanza Nyerere na Kigoma kitaitwa Mkapa.
"Reli ya Mwendokasi itakayotumia teknolojia ya kisasa ina manufaa makubwa ikiwemo kupunguza msongamano wa magari barabarani na kuongeza ufanisi katika usafiri," Amesema
Amesema, “Uzinduzi wa Reli ya Mwendokasi ni hatua kubwa kuelekea maendeleo endelevu. Mradi huu utaunganisha miji mikubwa na kuongeza fursa za ajira, huku ukichangia katika ukuaji wa uchumi wa taifa letu, "amesema
Pamoja na mambo mengine hafla hiyo ambayo ilihudhuriwa na viongozi wa serikali, wawakilishi wa sekta binafsi, na wananchi walitumia nafasi hiyo kuisifu juhudi zilizowekwa kuhakikisha kwamba mradi unakidhi viwango vya kimataifa.
" Reli ya Mwendokasi (SGR) imeanza rasmi kutoa huduma kwa umma na ina matarajio ya kuwa na ushawishi mkubwa katika kuboresha huduma za usafiri nchini na kutoa ajira zaidi ya elfu 30,"amesema Waziri wa uchukuzi Makame Mbarawa
Social Plugin