WAKAZI BUGURUNI KISIWANI WAPATA NAFUU MADENI HUDUMA ZA MAJI

 

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) Mkoa wa Kihuduma Ilala imeendesha zoezi la kuwatembelea Wateja mbalimbali waliositishiwa huduma za Majisafi kutokana madeni ya muda mrefu na kuanza hatua za kuwarudishia huduma kwa makubaliano maalum.

Meneja wa DAWASA Ilala Mhandisi, Honest Makoi wakati wa zoezi hilo lilofanyika mtaa wa Buguruni ameeleza kuwa utaratibu huo utaendelea katika maeneo mengine ili kuhakikisha wananchi wanatumia huduma za Mamlaka zenye usalama na unafuu zaidi.

"Tumekuja kuonana na Wateja wetu ambao awali walikuwa wanatumia huduma zetu na baadae kusitishiwa kutokana na madeni, tumezungumza nao ili kukubaliana kurudisha huduma kwa makubaliano ya kulipia taratibu kila mwezi maana huduma zetu ni salama na nafuu." alisema Mha. Makoi

Naye Ndugu Ramadhani Hashim Mkazi wa Buguruni Kisiwani ameshukuru kwa hatua ya DAWASA kuwatembelea kwa kuwa wamekuwa na changamoto ya kukosa huduma kutokana na madeni makubwa bila kujua hatima yao ya kurejeshewa huduma.

"Ni kweli DAWASA wanatudai lakini sasa kulipia kwa mara moja deni ni jambo gumu kwetu ukizingatia hali zetu ila nashukuru leo wamekuja na tumekubaliana ili tuendelee kupata huduma ya Majisafi” alisema Hashim

Jumla ya wateja 20 wametembeleawa na kurudishiwa huduma ya maji katika eneo la Buguruni Kisiwani

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post