Zoezi la ugawaji wa vifaa vya maunganisho mapya kwa wakazi wa maeneo ya Magomeni, Tandale, Mburahati, Kigogo, Ndugumbi, Ubungo, Makurumla na Mabibo ambao wamekamilisha taratibu za upatikanaji wa huduma ya majisafi, limetekelezwa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA).
Zoezi la kugawa vifaa hivyo limefanyika katika ofisi za DAWASA Magomeni ambapo wateja 62 wamepatiwa vifaa hivyo tayari kwa ajili ya kuunganishiwa na huduma ya Majisafi.
Sambamba na zoezi hilo, Mamlaka imetoa elimu ya utunzaji miundombinu ya maji, njia rasmi za kuwasiliana na Mamlaka na malipo ya ankara na huduma nyingine zitolewazo na DAWASA.
Social Plugin