NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
WANAHARAKATI wamepaza sauti zao kuhakikisha haki inatendekea kwa washtakiwa wanadaiwa kumbaka kwa kundi na kumlawiti binti aliyejitambulisha anatokea Yombo Dar es Salaam ambapo mpaka sasa kesi bado ipo mahakamani na watuhumiwa wameshakamatwa.
Wakitoa maoni yao leo Agosti 21, 2024 katika Semina za Jinsia na Maendeleo ambazo hufanyika kila Jumatano, wanaharakati hao wamesema jamii inatakiwa kujua kila hatua inayoendelea kama walivyofanya ukatili huo.
Wamesema kutokana kusemekana muhusika aliyewatuma watuhumiwa kufanya tukio hilo yupo basi anatakiwa kukamatwa na kujibu tuhuma hizo na pia kuchukuliwa hatua kama akikutwa na hatia ya kufanya kitendo hicho.
Aidha wamesema wameviomba vyombo husika kutoa taarifa sahihi kuhusu binti kuanzia alipo, na serikali kutengeneza NGO's yake itakayojenga na kumfariji binti huyo ambaye amefanyiwa ukatili.
Pamoja na hayo wanaharakati hao wameiomba jamii kuungana kwa pamoja kuhakikisha wanakemea vitendo vya ukatili ambavyo vimekuwa vikitokea mara kwa mara kwenye jamii ambayo inatuzunguka.