WATANO WAKAMATWA KWA TUHUMA ZA WIZI WA MASHINE


Na Mariam Kagenda _Kagera

Jeshi la polisi mkoani Kagera linawashikilia watu watano baada ya kukutwa na mashine 12 zinazotumika kwenye boti za kuvulia samaki na pikipiki sita ambazo wanadai ni mali za wizi ambazo ziliibiwa sehemu mbalimbali .
Kamanda wa jeshi hilo Blasius Chatanda alieleza hayo wakati akiongea na vyombo mbalimbali vya habari katika viwanja vya ofisi za jeshi hilo ambapo alisema waliweza kukamata vifaa hivyo kutokana na operesheni saka waalifu iliyofanyika ndani ya ziwa victoria na maeneo yote ya mkoa huo.

"Operesheni ilinza mwezi Juni mpaka Agosti 11 mwaka huu ambapo tulianzia ziwa victoria baada ya kupata taarifa ya uwepo wa wizi wa mashine zinazotumika kwa ajili ya kuvua samaki (Engene bort) kutoka kwa baadhi ya wananchi hususani wavuvi ambapo tumezikamatia mikoa ya Bariadi na Mara ambapo wamo walioiba na wanunuzi wa mali hizo za wizi"alieleza kamanda.

Wakati huo huo jeshi hilo linaendelea na ufuatiliaji wa tukio la uvunjaji wa maduka mawili ya huduma za kifedha eneo la Omulushaka Wilayani Karagwe ambalo lilihusisha watu kati ya sita hadi saba ambapo mmoja wa majambazi hao alifariki wakati akipelekwa hospitali baada ya kujeruhiwa kwa risasi katika majibizano na polisi.
Kamanda alisema tukio hilo lilitokea Agosti 9 mwaka huu saa saba usiku ambapo polisi walijulishwa wakati majambazi hao wakiendelea na uvunjaji huo na baada ya kufika eneo la tukio walikuta mlinzi akitokwa na damu nyingi baada ya kupigwa na kitu chenye ncha na anaendelea na matibabu na hari yake inaendelea vizuzi.

Alisema majambazi hao baada ya kuwaona polisi walianza kukimbilia mtoni upande wa mashariki wa eneo la Omulushaka huku wakiendelea kuwarushia polisi mawe kwa lengo la kuwakatisha tamaa wasiwafuatilie.

Katika tukio hilo waharifu hao walianza mapambano na polisi ambapo polisi walimpiga mmoja wao risasi ya mguu na kufanikisha kumkamata lakini alifariki wakati akipelekwa hospitali na imebainika kuwa alikuwa ametokea mkoani Geita mwenye umri kati ya miaka 25 hadi 30 na wenzake walitoroka wakiwa tayali wamepora kiasi cha shilingi milioni 11 na wanaendelea kusakwa na polisi.

Aidha Kamanda Chatanda aliwataka wanaojihusisha na uharifu kutambua kuwa mkoa wa Kagera si mahali pa kufanya vitendo hivyo wakijaribu watakamatwa na kuchukuliwa hatua kali za kisheria.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post