MWANASHERIA Mkuu wa Serikali Bw. Hamza Johari, amewataka watumishi wa ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kufanya kazi kwa weledi ili kuongeza ubora na ufanisi katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku ya kuwatumikia wananchi.
Bw. Johari amesema hayo jijini Dodoma wakati wa hafla fupi ya makabidhiano ya ofisi na aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali Jaji, Dk. Eliezer Feleshi iliyofanyika mji wa kiserikali Mtumba.
Alisema, watumishi wa ofisi yake wanapaswa kufanya kazi kwa weledi ili kuongeza ubora na ufanisi katika kuwahudumia wananchi wenye changamoto mbalimbali za kisheria.
“Niwaombe watumishi wa Ofisi ya Mwanasheria mkuu kufanya kazi kwa kuzingatia weledi ili kuongeza ubora na ufanisi wakati wa kutekeleza majukumu yenu ya kuwahudumia Watanzania”alisema Kwa upande wake, Jaji Dkt. Eliezer Mbuki Feleshi amewasisitizia Menejimenti na Watumishi wa Ofisi hiyo kutoa ushirikiano kwa Mwanasheria Mkuu na Naibu Mwanasheria Mkuu wakati wote ili kuongeza ufanisi.
Social Plugin