ZIARA YA RAIS SAMIA MOROGORO YAVUNA WAPINZANI 320 WAHAMIA CCM, WAPOLELEWA NA MBUNGE ABOOD

 
Na Christina Cosmas, Morogoro

Ikiwa ni siku chache tangu Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kumaliza ziara kubwa ya Siku 6 Mkoani Morogoro kwa kufungua miradi sambana na kukutana na Wananchi, Wapinzani wa Morogoro mjini wameshindwa kuvumilia na kuamua kuhamia Chama cha Mapinduzi (CCM).

Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Abdulaziz Abood amepokea wanachama wapya 320 kutoka vyama mbalimbali  vya Upinzani walioamua kwa hiari yao kujiunga na CCM mara baada ya kuridhishwa na kazi nzuri inayofanywa na serikali ya Rais Samia wakati Abood  akizindua Shina waliloanzisha wao la Wakereketwa wa Chama cha Mapinduzi Mawenzi Sokoni.


Abood amewapongeza wapinzani hao kwa uamuzi mzuri wa kuhamia CCM huku akipongeza juhudi za Rais Samia za kuwaletea watanzania maendeleo huku akidumisha upendo.


"Nimeshuhudia Juzi Mheshimiwa Rais alikuja Morogoro kututembelea, tumezungumza shida zetu na papohapo akazitatua, tumeomba hospitali ya rufaa katumwagia Bilion 5 palepale, tumemuomba maji mkataba wa bilioni 185 umecheleweshwa kusainiwa kamuelekeza Waziri mpaka Oktoba mkataba usainiwe, tumemuomba pesa za barabara, amemuelekeza Waziri atuongezee, hivyo tuna kila sababu ya kumshukuru Rais wetu na ndio maana leo wenzetu uvumilivu umewashinda", amesema.


Aidha Mbunge huyo amewapongeza Wafanyabiara wa soko la Mawenzi kwa umoja wao na shughuli kubwa na nzuri wanayoifanya ya kulisha Morogoro na kushiriki katika ujenzi wa nchi yao.

Hivyo Abood ameahidi kuendelea kutatua kero na changamoto za soko hilo huku akibainisha alivyochonga barabara za soko hilo zilizokuwa kero kubwa kwa wafanyabiashara hao na kueleza mafanikio waliyoyapata baada ya kupata eneo hilo kutoka posta mpaka Manispaa.


Nae Katibu wa idara ya Uenezi CCM Wilaya ya Morogoro Mjini  Maulid Chambilila amewakaribisha kwa kishindo kikubwa wanachama wapya kutoka upinzani akiwataka kutulia ndani ya CCM chama bora na sikivu kwa watu wake.

Wanachama hao wapya kutoka katika vyama vya upinzani wameeleza furaha yao kujiunga CCM hasa wakielekeza shukrani zao kwa Rais Samia kuwa wamefurahishwa na uchapa kazi wake huku akionesha kutatua kero za wananchi bila kuwa na ubaguzi na kuifanya nchi kuwa maendeleo endelevu.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post